Mkuu Mpya wa Mkmoa wa Mara, Adam Kigoma Malima
Mkuu wa Zamani wa Jeshi la Polisi Tanzania, Ernest Mangu, aliyeteuliwa kuwa Balozi.
****************
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 26
Oktoba, 2017 amefanya mabadiliko katika safi ya Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu
Wakuu na Wakuu wa Mikoa kwa kuteua, kupandisha vyeo na kuhamisha vituo vya
kazi.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es Salaam
imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameteua amewapandish Naibu Makatibu Wakuu 4 na
kuwa Makatibu Wakuu wapya, ameteua Naibu Makatibu Wakuu wapya 7 na amewahamisha
vituo vya kazi Makatibu Wakuu 4 na Naibu Katibu Mkuu 1.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 3 na kufanya mabadiliko
katika mikoa mingine 3. Na pia amefanya uteuzi wa Balozi mmoja.
Orodha
ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo;
1. Ofisi ya Rais Ikulu.
·
Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata
2. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora.
·
Katibu Mkuu (Utumishi) – Laurian
Ndumbaro
·
Naibu Katibu Mkuu - Dorothy Mwaluko
3. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
·
Katibu Mkuu - Mhandisi Mussa Iyombe
·
Naibu Katibu Mkuu(Afya) - Dkt. Zainabu Chaula
·
Naibu Katibu Mkuu(Elimu) - Bw. Tixon Nzunda
4. Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na
Mazingira.
·
Katibu Mkuu - Mhandisi Joseph Kizito Malongo
·
Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Phillipo
5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
·
Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
·
Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) - Maimuna Tarishi
6. Wizara ya Kilimo.
·
Katibu Mkuu -
Mhandisi Methew Mtigumwe
·
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Thomas Didimu Kashililah
7. Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
·
Katibu Mkuu (Mifugo) - Dkt. Maria
Mashingo
·
Katibu Mkuu (Uvuvi) - Dkt. Yohana
Budeba
8. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
·
Katibu Mkuu (Ujenzi) - Mhandisi
Joseph Nyamuhanga
·
Katibu Mkuu (Uchukuzi) - Dkt. Leonard
Chamriho
·
Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria Sassabo
·
Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina Madete
9. Wizara ya Fedha na Mipango.
·
Katibu Mkuu -
Doto James Mgosha
·
Naibu Katibu Mkuu (Utawala) - Bi. Susana
Mkapa
·
Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina Shaaban
·
Naibu Katibu Mkuu (Sera) - Dkt. Khatibu Kazungu
10.Wizara
ya Nishati.
·
Katibu Mkuu - Dkt. Hamis Mwinyimvua
11.Wizara
ya Madini.
·
Katibu Mkuu -
Prof. Simon S. Msanjila
12.
Wizara
ya Katiba na Sheria.
·
Katibu Mkuu -
Prof. Sifuni Mchome
·
Naibu Katibu Mkuu - Amon Mpanju
13.
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
·
Katibu Mkuu - Prof. Adolf F. Mkenda
·
Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi
14.Wizara
ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
·
Katibu Mkuu -
Dkt. Florence Turuka
·
Naibu Katibu Mkuu - Bi. Immaculate Peter Ngwale
15.
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
·
Katibu Mkuu -
Meja Jen. Projest A. Rwegasira
·
Naibu Katibu Mkuu - Balozi Hassan Simba Yahaya
16.Wizara
ya Maliasili na Utalii.
·
Katibu Mkuu - Meja Jen. Gaudence S. Milanzi
·
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Aloyce K. Nzuki
17.Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
·
Katibu Mkuu - Dorothy Mwanyika
·
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Moses M. Kusiluka
18.Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
·
Katibu Mkuu -
Prof. Elisante Ole Gabriel
·
Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye
·
Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija
19.
Wizara
ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
·
Katibu Mkuu -
Dkt. Leonard Akwilapo
·
Naibu Katibu Mkuu - Prof. James Epiphan Mdoe
·
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Ave-Maria Semakafu
20.
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
·
Katibu Mkuu (Afya) - Dkt. Mpoki Ulisubisya
·
Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto) - Bi. Sihaba
Nkinga.
21.
Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
·
Katibu Mkuu -
Bi. Suzan Paul Mlawi
·
Naibu Katibu Mkuu - Nicholaus B. William
22.
Wizara
ya Maji na Umwagiliaji.
·
Katibu Mkuu - Prof. Kitila Mkumbo
·
Naibu Katibu Mkuu - Mhandisi Emmanuel Kalobelo
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amewapandisha vyeo Wakuu wa Wilaya 3 na kuwateua kuwa Wakuu
wa Mikoa kujaza nafasi za Wakuu wa Mikoa waliostaafu.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Bw. Alexander Pastory Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Manyara. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mnyeti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru na
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Joel Bendera ambaye amestaafu.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Bw. Joackim Leonard Wangabo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Wangabo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na anachukua
nafasi ya Kamishna wa Polisi Zelote Stephen ambaye amestaafu.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Gabriel Luhumbi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Kabla ya uteuzi huu Bw. Luhumbi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na anachukua
nafasi ya Meja Jen. Ezekiel Kyunga ambaye amestaafu.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Bw. Adam Kigoma Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. Bw.
Adam Kigoma Malima anachukua nafasi ya Dkt. Charles Mlingwa.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Bi. Christine Solomon Mndeme kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma. Kabla ya uteuzi huu Bi. Mndeme alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini
na anachukua nafasi ya Bw. Jordan Rugimbana.
Mhe.
Rais Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gasper Byakanwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara. Bw. Byakanwa alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na anachukua nafasi ya Bi.
Halima Dendego.
Katika hatua nyingine,
Mhe. Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP - Mstaafu) Ernest Mangu kuwa Balozi.
IGP
– Mstaafu Ernest Mangu pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima watapangiwa vituo
vya kazi baada ya taratibu kukamilika.
Makatibu
Wakuu wapya 4, Naibu Makatibu Wakuu wapya 7, na Wakuu wa Mikoa 6 walioteuliwa wataapishwa
kesho tarehe 27 Oktoba, 2017 saa 8:00 Mchana, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment