Wanafunzi wa Chuo cha Bahari
nchini (DMI) wakielea majini huku wameshikilia boya kubwa la kujiokolea lenye
uwezo wa kushikwa na watu 12 wakati wa zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia
kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya
ajali. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo
cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa
lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi
inapotokea dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Mwanafunzi kutoka Chuo cha Bahari
nchini (DMI) akiruka kwenye maji huku akitazamwa na baadhi ya abiria wa kivuko
cha MV. KAZI wakati wa zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia kivuko cha
Magogoni Kigamboni jinsi ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya ajali. Zoezi
hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo cha Habari na
Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa lengo la
kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Wanafunzi wa Chuo cha Bahari
nchini (DMI) wakielea majini huku wameshikilia boya kubwa la kujiokolea lenye
uwezo wa kushikwa na watu 12 wakati wa zoezi la kuwafundisha abiria wanaotumia
kivuko cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kujiokoa pindi inapotokea dharura ya
ajali. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Kitengo
cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha Magogoni Kigamboni kwa
lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea dharura watumiaji wa vivuko
hivyo.
Abiria waliokua katika kivuko cha
MV. MAGOGONI wakimuangalia mmoja wa wazamiaji wakati akirukia kwenye maji
katika zoezi la kuwafundisha jinsi ya kuingia majini pindi inapotokea dharura
ya ajali katika kivuko. Zoezi hilo lililoandaliwa na Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Kitengo cha Habari na Mawasiliano limefanyika katika kivuko cha
Magogoni Kigamboni kwa lengo la kuwapa elimu ya kujiokoa pindi inapotokea
dharura watumiaji wa vivuko hivyo.
Na Alfred Mgweno-Temesa
Wanafunzi kutoka chuo cha
Bahari nchini (DMI) leo wamefanya zoezi la kufundisha abiria wanaotumia kivuko
cha Magogoni Kigamboni jinsi ya kutumia vifaa vya kujiokolea vilivyomo katika
vivuko hivyo pindi inapotokea dharura ya ajali kwenye maji.
Zoezi hilo lililoratibiwa na
chuo cha Bahari kwa kushirikiana na kitengo cha Habari na Mawasiliano (TEMESA)
limefanyika kivukoni hapo mapema asubuhi likiongozwa na Nahodha Nyamurasa Matage
kutoka chuo hicho. Zoezi hilo lilihusisha wanafunzi wa kozi ya PST na lilikua
na nia ya kuwaonyesha watumiaji wa kivuko hicho namna ya kujiokoa na pia
kujifunza kuwa na utulivu pindi inapotokea dharura ya ajali, moto au kuzimika
kwa kivuko.
Akizungumza katika tukio hilo
Nahodha Nyamurasa aliwataka watumiaji wa kivuko hicho kuhakikisha wanafuatilia
kwa makini zoezi hilo kwani dharura ya ajali inaweza kutokea wakati wowote na
mahala popote hivyo abiria wanatakiwa kuwa watulivu pindi inapotokea. Alisema mafunzo
hayo yalikua ni sehemu ya masomo yao ya darasani lakini pia elimu tosha kwa
watumiaji wa vivuko.
Naye Mkuu wa kivuko Magogoni
Kigamboni Mhandisi Lukombe King’ombe akizungumza wakati wa zoezi hilo aliwataka
wanafunzi hao kulichukulia kwa umakini zoezi hilo kwani pindi wanapomaliza
mafunzo yao wanatumiwa katika vivuko vya TEMESA katika shughuli za uokoaji wa
abiria na mali zao na pia kutoa maelekezo ya usalama kwa abiria wa vivuko hivyo,
“hili ni zoezi muhimu kwa abiria wetu kulipata na kujifunza namna ya kutumia
vifaa vya kujiokolea ambavyo vinakuwepo muda wote katika vivuko vyetu”,
alisema.
Dhumuni kubwa la zoezi hilo
lilikua ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo hicho na pia kutoa mafunzo kwa
abiria wanaotumia kivuko. Zoezi hilo linategemewa kuendelea wiki ijayo katika
kivuko hicho.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment