Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 25 February 2017

RAIS MUSEVENI WA UGANDA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI NCHINI TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili. Amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Mapokezi yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili. Amepokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Mapokezi yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtabulisha kwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakisimama kwa nyimbo za Taifa mgeni alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017


Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akikagua gwaride alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitambulishwa kwa ujumbe wa Uganda na  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wakiandgalia ngoma za utamaduni mgeni alipowasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni  wakiwasili Ikulu jijini Dar es salaam tayari kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia wakati mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akipiga ngoma alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu  jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu  jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017 PICHA NA IKULU


Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara jijini Abidjan

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 23Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Ivory Coast, Mhe. Alassane Ouattara katika Ikulu yake jijini Abidjan.Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu.

Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Ouattara wamezungumzia hali ya elimu bara la Afrika na Ivory Coast kwa ujumla na haja ya kufanya mageuzi makubwa katika elimu ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.
Rais Mstaafu Kikwete amempongeza Rais Outtara kwa jitihada kubwa anayoifanya kuinua elimu nchini mwake. Kwa mujibu wa utafiti wa Kamisheni, Ivory Coast iko katika nafasi nzuri ya kufikia viwango vya juu vya ubora wa elimu vya nchi zilizoendelea iwapo itaongeza juhudi ya kufanya mageuzi kulingana na mapendekezo ya Kamisheni hiyo.

Rais Outtara amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini mwake. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Akiwa jijini Abidjan, Rais Mstaafu ametembelewa na viongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika na Watoto  wa Watanzania hao ambao walitaka kujua kuhusu masuala ya uongozi na maisha baada ya kustaafu. 
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya 'Kizazi cha Elimu' Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Rais Alassane Ouattara baada ya mazungumzo yao   Ikulu ya Ivory Coast.

 Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake Abidjan
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia autograph  watoto waliomtembelea hotelini kwake  jijini Abidjan


Friday, 24 February 2017

MSIKILIZE MZEE MWINYI AKISEMA JINSI GANI YUPO FITI


RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AWATOA HOFU WATANZANIA NA KUSEMA YUPO FITI

Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza hii leo na kukasema watanzania wasiwe na hofu juu ya afya yake.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, wakati Mzee Mwinyi alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam jana.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, wakati Mzee Mwinyi alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Upanga Dar es Salaam jana.


Na Mroki Mroki
Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi amezengumza na TSN Digital na kuwatoa hofu watanzania juu ya afya yake na kusema kuwa yupo vizuri na wala hasumbuliwi na maradhi yoyote.

Rais Mstaafu Mwinyi alizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati alipomtembelea na kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya, nyumbani kwake Upanga hii leo.

“Ah Mimi niko vizuri nina afya njema na leo nimefanya mazoezi yangu kama kawaida kwa kutembea kilometa tano kwa mwendo wa kasi, hivyo niwatoe hofu watanzania na wananchi kwa ujumla juu ya afya yangu,”alisema Alhaji Mwinyi.

Jana katika mitandao ya kijamii kulienezwa tarifa kutoka nchini Marekani ambako walisema Rais huyo alikuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo na kufariki Dunia jambo ambalo si la kweli na kiongozi huyo yupo mwenye afya njema.

Aidha tarifa kutoka idara ya Habari Maeleozo kupitia Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas ilikanisha tarifa hizo na kusema kuwa Mzee Mwinyi ni mzima wa afya, anaendelea na majukumu yake kama kawaida.

“Jana alihudhuria chakula cha jioni kuadhimisha siku ya Taifa la Kuwait na leo mchana baada ya swala ya Ijumaa alimtembelea kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya,”ilisema tarifa hiyo.

Dk Abbasi aliitaka jamii ifahamu kuwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015, kwa mtu yeyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari za uongo au uzushi katika mitandao.


Thursday, 23 February 2017

BAADA YA KIPINDUPINDU KUINGIA KIGAMBONI, MBUNGE DK FAUSTINE NDUNGULILE ATOA ELIMU KWA WANANCHI WAKE

TAARIFA
Kipindupindu kimeingia kwenye Wilaya ya Kigamboni. Napenda kuwakumbusha wananchi wa Kigamboni kuzingatia kanuni za afya ikiwa ni pamoja na:

1. Kutumia maji yaliyochemshwa
2. Kutumia maji ya visima vifupi kwa tahadhari
3. Kula vyakula vya moto na kuepuka vyakula vya mitaani
4. Kuchukua tahadhari katika kuhudumia mgonjwa anayeharisha
5. Kuepuka vyakula vilivyopoa kwenye mikusanyiko ya watu
6. Kutotupa taka ovyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni imeshachukua hatua zifuatazo:
1. Imeshaandaa wodi maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu
2. Kuchukua sampuli toka baadhi ya vyanzo vya maji
3. Kutibu baadhi ya vyanzo kwa kutumia klorini
4. Kufukia baadhi ya visima vifupi ambavyo vimethibitika kutokuwa salama
5. Kusimamia kanuni za afya
6. Kutoa elimu kwa umma.

Natoa rai kwa wananchi wote wa Kigamboni kuchukua tahadhari ili tuweze kudhibiti ugonjwa huu.
Naomba tusambaze taarifa kwa wana Kigamboni wengine.
Asanteni




Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge-Kigamboni
23.02.2017


RAIS DKT. MAGUFULI AMSAIDIA DADA NEEMA MWITA WAMBURA ALIYEMWAGIWA UJI WA MOTO NA MUMEWE MKOANI MARA.


RAIS DKT. MAGUFULI AMSAIDIA DADA NEEMA MWITA WAMBURA ALIYEMWAGIWA UJI WA MOTO NA MUMEWE MKOANI MARA.

Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni  kitendo kilichofanywa na mume wake.



Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura na Ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza kuhusu hali ya mgonjwa Dada Neema Mwita Wambura (32) aliyefikishwa tena katika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.

Daktari Bingwa wa upasuaji wa ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  Dkt. Ibrahim Mkoma akizungumzia historia ya mgonjwa huyo ambaye yeye pamoja na jopo la madaktari bingwa walimfanyia upasuaji ili kutibu majeraha yake ya ngozi katika kipindi cha nyuma.
Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano.  Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.



Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.



Dada Neema Mwita Wambura (32) wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.



Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni  kitendo kilichofanywa na mume wake.
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema Mwita Wambura (32) mara baada ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada Neema Mwita alifanyiwa upasuaji mara nne katika siku za nyuma hospitalini hapo Muhimbili ili kutibu majeraha yake hayo ya moto.