Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 20 June 2018

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AWAONYA WANASIASA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU  WAJIBU WA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA KUTII SHERIA ZA NCHI ILI KUKUZA DEMOKRASIA NA AMANI YA NCHI
 
Nachukua fursa hii kuwaasa Viongozi wote wa Vyama vya Siasa na wanachama kutekeleza majukumu yao ya kisiasa kwa kufuata na kuzingatia Sheria na Kanuni za Vyama vya Siasa na Sheria za nchi kwa ujumla.

Kufuatia tabia iliyojitokeza ya baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kutumia vibaya vyombo vya habari, hususani mitandao ya kijamii kufanya vitendo au kutoa kauli ambazo zinavunja sheria za nchi, ni wito wangu kwao kuacha tabia hiyo mara moja.

Ninasisitiza kuwa Viongozi wa Vyama vya Siasa wasitumie vibaya dhana ya demokrasia na uhuru wa habari, kuvunja Sheria za nchi. Ieleweke kwamba mtu yeyote anapokiuka sheria za nchi, Sheria itachukua mkondo wake bila kujali wadhifa wa mhusika katika chama cha siasa.

Rai yangu kwa Viongozi wote wa Vyama vya Siasa na wanachama wote wa vyama vya siasa nchini, ni wajibu wa kila mmoja wao kuelewa kwamba katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa wanapaswa kuheshimu Sheria za nchi wakati wote ili kudumisha na kukuza demokrasia ya vyama vingi nchini. Kwa kufanya hivyo pia, Viongozi hawa watalinda na kuimarisha Amani ya nchi yetu.

 
  Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA


WAZIRI LUKUVI ATENGUA UTEUZI WA MCHECHU NHC


TAARIFA NZIMA YA WAZIRI MPINA KUHUSU KUKAMATWA KWA SAMAKI BUNGENI HII HAPA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akitoa taarifa ya serikali kuhusu tukio la kukamatwa kwa samaki wachanga wasioruhusiwa kisheria katika mgahawa wa Bunge Juni 19,2018.


Thursday, 14 June 2018

HII HAPA HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI 2018/2019

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akionesha mkoba ulio na nyaraka za Bajeti ya serikali ya 2018/2019


Monday, 11 June 2018

SERIKALI: HAKUNA MFUKO MAALUM WA KUHIFADHI FEDHA ZA KULIPA DENI LA TAIFA

Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Serikali imesema kuwa hakuna akiba ya fedha iliyowekwa katika mfuko maalum kwa ajili ya kulipia Deni la Taifa kwa sababu deni hilo linajumlisha Deni la Serikali na Deni la Sekta Binafsi, lakini Serikali inalipa deni lake pekee bila kuhusisha deni la Sekta Binafsi.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa Akijibu maswali ya Mbunge wa Mtambile Mhe. Masoud Abdallah Salim aliyetaka kujua Deni la Taifa limefikia kiasi gani na namna mchanganuo wa fedha zilizowekwa akiba kwa ajili ya kulipa deni hilo ulivyo.

“Fedha kwa ajili ya malipo ya Deni la Serikali inatengwa kwa kuzingatia taratibu za kawaida za kibajeti kupitia Fungu 22, katika Mwaka wa Fedha 2017/18, Serikali ilitenga kiasi cha Sh. trilioni 1.262 kwa ajili ya malipo ya deni la ndani na Sh. bilioni 685.06 kwa deni la nje”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu Deni la Taifa limefikia Dola za Marekani milioni 26,161.02 sawa na zaidi ya Shilingi trilioni 59.4

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge huyo aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha Deni la Taifa linahakikiwa ili kujua kama Serikali inakopesheka au la, Dkt. Kijaji alilihakikishia Bunge kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha, Deni la Taifa litahakikiwa kama nchi nyingine zinavyofanya kwani mkataba wa kuhakiki deni hilo upo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hatua za mwisho.

Waziri huyo alisema kuwa Deni la Taifa ni himilivu na Serikali imekuwa makini katika ulipaji kwa kuhakikisha inalipa kila mwezi madeni katika Taasisi zote ilizokopa hali inayoifanya nchi kuaminika na Taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa

Aidha, Mhe. Kijaji alifafanua kuwa fedha zote zinazokopwa zinapelekwa katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi ili kuendelea kuinua uchumi wa nchi hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa viwanda.


Tuesday, 5 June 2018

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.


Majaji watatu walioapishwa wakila Kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali akifatiwa na Jaji Mwanaisha Athuman pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi 


Majaji pamoja na watendaji wa Mahakama Kuu pamoja na Mahakama ya Rufani wakifatilia tukio la uapisho wa Majaji watatu Ikulu jijini Dar es Salaam.


Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali akizungumza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji watatu aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali pamoja na Jaji Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
x


MUKTASARI WA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA 2018/19

Waziri wa Fedha na Mipango. Dk. Philip Mpango


BUNGENI JIJINI DODOMA LEO

WANAFUNZI wa Kidato cha Tano wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi. Picha;Mroki Mroki/Daily News Digital-Dodoma

WANAFUNZI wa Kidato cha Tano wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi.
WANAFUNZI wa Kidato cha Tano wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi.
Wanachuo kutoka Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) wakiwa Bungeni kwa ziara ya kimafunzo.


Wanachuo kutoka Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) wakiwa Bungeni kwa ziara ya kimafunzo.


WANAFUNZI wa shule ya Mt Everist ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi.

WANAFUNZI wa shule ya Mt Everist ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi.

WANAFUNZI wa Kidato cha Tano wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi.


WANAFUNZI wa Kidato cha Tano wa Shule ya Sekondari ya Tusiime ya Jijini Dar es Salaam wakiwa Bungeni jijini Dodoma jana kwa ziara ya kimafunzo. Ambapo walishuhudia shughuli mbalimbali za Bunge na namna Bunge linavyofanya kazi.


Maofisa mbalimbali kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi zake wakiwa Bungeni jijini Dodoma wakati Bajeti ya Wizara yao ikisomwa na kujadiliwa.


SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI WA MAFAO YA WATUMISHI KABLA YA PSPF

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa watumishi wote wa Serikali Kuu walioajiriwa na kuthibitishwa katika ajira ya masharti ya kudumu na pensheni, kabla ya mwaka 1999 waliunganishwa katika Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa mujibu wa Sheria.

Hayo yameelezwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum,  Lucy Mlowe aliyetaka kujua Serikali inawafikiriaje watumishi wa Sekta ya Afya walioajiriwa na Serikali Kuu miaka ya 1980 ambao fedha zao hazikukatwa na mfuko wa hifadhi ya jamii.

Dkt. Kijaji, alisema kuwa Kabla ya Julai 1999 mfumo wa malipo ya mafao ya kustaafu kwa watumishi wa Serikali Kuu haukuwa wa kuchangia hivyo watumishi wote waliokuwa kwenye ajira ya masharti ya kudumu wanastahili malipo ya uzeeni wakiwemo watumishi wa Sekta ya Afya hata bila kuchangia.

“Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Sheria ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, watumishi wote wa Serikali Kuu ambao waliajiriwa na kuthibitishwa katika ajira ya masharti ya kudumu na pensheni wanakuwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF kuanzia tarehe ya kuanzishwa kwa mfuko”, alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi Na. 2 ya mwaka 1999 kwa watumishi wa umma ambayo ilianzisha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wastaafu wote ambao ni wanachama wa Mfuko huo na wanaguswa na sheria hii wanalipwa mafao ya kustaafu na mfuko huo kwa kipindi chao chote cha utumishi.

Dkt. Kijaji alibainisha kuwa mafao ya watumishi yanakokotolewa kuanzia tarehe ya kuajiriwa hadi wanapostaafu utumishi wao kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.