Rais
Dkt John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Adelardus Kilangi (pichani) kuwa Mwanasheria Mkuu
wa Serikali (AG).
Taarifa
iliyotolewa jioni hii na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
uteuzi wa Dkt. Adelardus Kilangi umeanza Februari 1, 2018.
Kabla
ya uteuzi huu Dkt. Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu
Agustino (St. Augustine University)
kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (Tanzania
Petroleum Upstream Regulatory Authority – PURA).
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua, Paul Joel Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu
wa Serikali (DAG) kuanzia leo Februari 1, 2018.
Kabla
ya Uteuzi huu, Ngwembe alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania
Insurance Regulatory Authority – TIRA).
Kufuatia
uteuzi huu,Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Mcheche Masaju na aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama Kuu kuanzia Februari 1, 2018.
Wateule
wote wataapishwa Jumamosi Februari 03, 2018 saa 9:00 Alasiri.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment