Rais
Dkt. John Magufuli akimsikiliza Balozi mteule wa Ugiriki hapa nchini
Konstantinos Moatsos wakati alipokuwa akijitambulisha kabla ya kuwasilisha Hati
zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli
akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Mali hapa nchini Fafre Camara
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli akimtambulisha Waziri wa Mambo
ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa Balozi wa Ethiopia hapa nchini Dina
Mufti Said Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ethiopia hapa nchini Dina Mufti
Said Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli
akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Argentina hapa nchini Martin
Gomez Bustillo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Magufuli
akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufilipino hapa nchini Uriel
Norman Garibay Ikulu jijini Dar es Salaam
**************
RAIS
Dkt. John Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mabalozi 6
walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Mabalozi
waliowasilisha hati zao leo, Ikulu jijini Dar es Salaam ni Konstantinos Moatsos
– Balozi wa Ugiriki hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Fafre
Camara – Balozi wa Mali hapa nchini mwenye makazi yake Addis Ababa nchini
Ethiopia na Dina Mufti Sid – Balozi wa Ethiopia hapa nchini mwenye makazi yake
Nairobi nchini Kenya.
Wengine
ni Elizabeth Taylor – Balozi wa Colombia hapa nchini mwenye makazi yake Nairobi
nchini Kenya, Martin Gomez Bustillo – Balozi wa Argentina hapa nchini mwenye
makazi yake Nairobi nchini Kenya na Uriel Norman Garibay – Balozi wa Ufilipino
mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya.
Rais
Magufuli amewapongeza Mabalozi wote kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa
nchini na ameahidi kuwapa ushirikiano utakaowezesha uhusiano na ushirikiano
kati ya Tanzania na nchi zao kukua zaidi.
Rais
Magufuli amewahakikishia kuwa Tanzania inatambua uwepo wa fursa mbalimbali za
kibiashara na kiuchumi katika nchi hizo pamoja na ujuzi na uzoefu katika nyanja
mbalimbali, na kwamba ni matarajio yake kuwa ujio wao utasaidia kuongeza
manufaa ya kiuchumi na kubadilishana uzoefu.
Pia
Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kufikisha salamu zake kwa viongozi wa nchi
zao na amewakaribisha kutembelea Tanzania.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment