Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa
ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo kwenye mafunzo ya maandalizi
ya Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.
Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa
ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo hilo kwenye mafunzo ya maandalizi
ya Uchaguzi Mdogo wa Februari 17, 2018.
Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kinondoni Boniface Lihamwike akiwaapisha wasiamamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa
Jimbo la Kinondoni na kata zake wakati wa mafunzo ya maandalizi ya Uchaguzi
Mdogo.
Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge, akiwasilisha
Mada ya Maelekezo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata
kwa wasiamamizi wa Kinondoni.Picha na
Hussein Makame-NEC
***************
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha wasimamizi wasaidizi wa
Uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia uchaguzi ili
kufanikisha Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Februari 17, 2018.
Hayo yamsemwa na Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Uchaguzi Kanda ya Pwani kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Stephen Elisante wakati akifungua mafunzo kwa
Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo la Kinondoni na Kata za jimbo
hilo la jiji la Dar es Salaam.
Alisema wasimamizi wa Uchaguzi wanapaswa kutambua kuwa Uchaguzi ni
mchakato unaohusisha taratibu mbalimbali kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni,
taratibu, maelekezo na miongozo iliyotolewa kisheria.
“Hivyo mnapaswa kuzisoma sheria hizo ili kuweze kutekeleza majukumu yenu
kwa mujibu wa sheria...,tufanye maamuzi yetu kwa kujitambua, kujiamini na
kutoogopa na kuchukua hatua za haraka katika kushughulikia changamoto
zinazojitokeza” alisema Elisante.
Aliwakumbusha wasimamizi hao wa Uchaguzi kuwa Tume imekuwa ikisisitiza
kwamba Sheria za Uchaguzi hazikuacha ombwe katika kueleza jinsi gani masuala ya
Uchaguzi yanatakiwa yatatuliwe.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni, Victoria Wihenge akiwasilisha
mada ya Maelekezo kwa wasimamizi hao, aliwataka kutoruhusu matumizi ya
utambulisho mwingine mbadala tofauti na ule ambao Tume ya Taifa ya Uchaguzi
imeruhusu kutumika.
“Kwa mujibu wa kifungu cha 61 (3) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi
Sura ya 343 na kifungu cha 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa
Sura ya 292, kimeipa mamlaka Tume kuidhinisha matumizi ya utambulisho mwingine
tofauti iwapo mpiga atakosa kadi ya kupigia kura” alisema Victoria na
kusisitiza kuwa:
“Vitambulisho vilivyoruhusiwa na Tume ni vitatu, Kitambulisho cha Taifa,
Hati ya Kusafiria kwa maana ya Passport na Leseni ya Udereva, hivyo mtu akikosa
kadi ya kupigia kura au vitambulisho hivyo hakuna utambulisho wowote
utakaoruhusiwa ili mtu aweze kupiga kura”
Mafunzo hayo kwa wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi kwa ngazi ya Jimbo la
Kinondoni na kata zilizoko kwenye jimbo hilo, yalijumuisha viapo kwa
wasiamamizi hao walioapa kutunza sira na kujivua au kukiri kuwa si mwanachama
wa chama chochote cha siasa.
Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Kinondoni pamoja na Jimbo la
Siha na Udiwani katika kata 10 za Tanzania, unatarajiwa kufanyika tarehe 17
Februari mwaka 2018.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment