KURUGENZI ya
Mawasiliano ya Rais inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli hatakuwa mgeni rasmi katika kongamano la maadhimisho ya kumbukizi
ya Mwalimu Nyerere kama inavyotangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya
kijamii.
Tarehe 11 Oktoba,
2017 ambayo inatangazwa kuwa ndio siku ya kufanyika kwa kongamano hilo, Mhe.
Rais atakuwa na majukumu mengine ya Kitaifa kulingana na ratiba yake ya kazi.
Taasisi mbalimbali
za umma na zisizo za umma zinazomualika Mhe. Rais katika shughuli zao
zinakumbushwa kutokutangaza ushiriki wa Mhe. Rais katika shughuli zao mpaka
zipate uthibitisho kutoka ofisi ya Rais.
Tafadhali tuzingatie
utaratibu huu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment