Waziri Mkuu. Kassim
Majaliwa akishiriki kupanda mbegu za miwa katika Shamba la Gereza Mbigiri kwa ajili ya maandalizi ya
kufufua Kiwanda cha Sukari na Kilimo cha miwa katika Gereza la Mbigiri Mkoani
Morogoro jana Septemba 2, 2017.
***************
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watendaji katika mikoa yote nchini
kuhakikisha wanafuatilia maendeleo ya viwanda mbalimbali katika maeneo
yao.
Amesema
mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda unalenga kuinua uchumi
wa Taifa kutoka wa chini kwenda wa kati, hivyo ni muhimu kuvifuatilia.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumamosi, Septemba 2, 2017) alipozungumza
na watendaji na wananchi wa mkoa wa Morogoro alipofanya ziara katika
kiwanda cha Moproco.
Alisema
licha ya kukuza uchumi wa Taifa, viwanda vitasaidia katika kutatua
tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana kwani vinauwezo wa
kuajiri watu wengi.
“Viwanda
hivi vinatupa uhakika wa ajira nchini kwa sababu vinauwezo wa kuajiri
watu wengi na wa kada mbalimbali, hivyo ni muhimu tukafuatilia utendaji
wake.”
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa mbali na kutoa ajira nyingi, pia viwanda
vitawezesha wakulima kupata soko la uhakika la mazao yao na kukifanya
kilimo kuwa na tija.
Alisema
kwa muda mrefu sekta ya viwanda nchini ilikuwa haifanyi vizuri jambo
ambalo lilisababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa
soko.
Hata
hivyo Waziri Mkuu alitoa wito kwa wafanyakazi walioajiriwa katika
viwanda mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo
kuendelea na uzalishaji.
Pia
aliwataka wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ili
kuviwezesha viwanda kuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi ndani ya
chini.
Awali Meneja
Mkuu wa kiwanda cha Moproco, Bw. Arif Abood aliiomba Serikali kuongeza
kodi kwa mafuta yanayotoka nje ya nchi ili kulinda viwanda vya ndani.
Alisema
uingizwaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kwa kiasi kukubwa ulichangia
kufungwa kwa viwanda vya ndani vya mafuta kutokana na kukosa soko.
Katika
ziara hiyo Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu na Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage pamoja na maofisa
wengine wa Serikali.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment