Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 2 August 2017

UWEKEZAJI ZAIDI WAHITAJIKA KATIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA

Mkuu wa Utawala na Maendeleo ya Uwezeshaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Danford Sango akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
PAMOJA na serikali kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, ikiwa ni asilimia 17 ya bajeti nzima, mazingira ya kufundisha na kufundishwa nchini bado si mazuri. Akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam pamoja na kuwekwa maeneo ya kuangaliwa kwanza ipo haja ya kufanya zaidi ili kufikia malengo. Dk Katabaro katika mada yake alisema kwamba pamoja na serikali kutenga zaidi ya TZS 1.366,685,241,000.00 katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi huku Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI) ikipatiwa sh 201,655,446,000/- kwa ajili ya elimu, alisema kwamba anaona ipo haja ya kuongeza nguvu katika maeneo kadhaa ili kuweka sawa mazingira ya kufundisha na kufundishwa.
 Katika mjadala huo wa kitaifa uliodhaminiwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Katabaro alisema kwamba kwa sasa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinakosekana katika shule nyingi na taasisi zinazohusiana na elimu na hivyo kukwamisha ufanisi na tija katika elimu. Aidha katika mada yake alitaka juhudi inayofanywa ya kuweka sawa mizania ya walimu pale walipo wengi kuhamishwa inabidi iendelee ili kuweka uwiano sawa wa elimu nchini. Pia alisema kuwa uwiano wa sasa wa walimu nchini sio sawa huku katika masomo, baadhi yakiwa na walimu wa ziada na mengine yakiwa na upungufu mkubwa. Profesa wa Menejimenti ya Elimu kutoka Skuli ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Eustella Bhalalusesa (katikati) akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha muwasilisha mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption] Mwaka 2016 kwa mujibu wake kulikuwa na walimu wa ziada katika masomo kadha huku kukiwa na upungufu katika masomo mengine hasa Hesabu na Sayansi: Basic Mathematics – 7,291 (Upungufu);Biolojia – 5181 (Upungufu);Kemia – 5373 (Upungufu);Fizikia – 6873 (Upungufu);Kilimo 508 (Upungufu);Kingereza– 1267 (ziada); Jiografia – 3281 (ziada); Historia – 4764 (ziada) na Kiswahili – 4795 (ziada). Pamoja na masomo Dk. Katabaro aliangalia bajeti hiyo katika maeneo muhimu yanayofanya mtoto kuwa na akili kama viwanja vya michezo na upatikanaji wa maji safi kwa ajili ya kunywa na usafi. Maji haya ni muhimu sana kwa watoto wa kike ambao usafi wao ndio siri ya mahudhurio ya shule kila siku. Dk Joviter Katabaro kutoka Skuli ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya elimu baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption] Mada hiyo pia ilitahadharisha kuhusu takwimu ikitaka zitumike vyema ili kuondoa mipango mibovu hasa ya uandikishaji wa watoto wa darasa la kwanza na wale wanaoingia kidato cha kwanza. Wakati huo huo katika mada iliyowakilishwa kwa pamoja kati ya Profesa haidari Amani na John Shilinde, kilimo pamoja na kutegemewa na wengi na kuwa chachu ya maendeleo ya viwanda bajeti yake iliyotengwa bado ni ndogo Walisema kwamba sekta hiyo ilipata kiasi cha karibu asilimia 10 ya bajeti nzima, bajeti ambayo ukiiangalia utaona kwamba haiwezi kubadili kilimo. Wamesema kwamba kilimo ambacho huajiri asilimia 70 ya wananchi ikichangia asilimia 28 ya pato la taifa huku ikipatia asilimia 30 ya mapato ya kigeni na kuchangia asilimia 65 ya mali ghafi, bado sekta haijapewa nguvu za kutosha kusonga mbele. Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo, Peter Lanya akizungumza machache kabla ya kumkaribisha muwasilishaji mada (hayupo pichani) kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.[/caption] Wamesema kilimo kitabadilika kwa fedha za utafiti na sayansi na ubunifu ili kuiweka sekta katika hali bora zaidi. Walisema kwamba sayansi na ubunifu ni kichocheo kikubwa cha mabadiliko katika kilimo. Wataalamu hao walitaka bajeti zaidi kwa ajili ya utafiti na maendeleo, kilimo cha umwagiliaji, kuongeza ruzuku, kuboresha kilimo cha kisasa cha kutumia zana kupunguza upotevu wa mazao baada ya mavuno, kuongeza kazi zenye staha vijijijni, kuongeza mnyororo wa thamani na matumizi endelevu ya ardhi na maji. Mtafiti Mshiriki Mwandamizi kutoka ESRF, John Shilinde akiwasilisha mada kuhusu bajeti ya kilimo baada ya kupitishwa Bungeni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Hildegalda Mushi kutoka COSTECH akichangia maoni kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mshiriki William Mhoja akichangia mada kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam Mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, Prof Honest Prosper Ngowi akishiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni sehemu ya wadau wa kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Picha ya pamoja ya wadau walioshiriki kwenye kongamano la siku moja la majadiliano ya kitaifa ya bajeti ya serikali 2017/18 katika elimu na kilimo lililoandaliwa na ESRF mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment