Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya ushirikiano wa kutangaza vivutio vya utalii baina ya Tanzania na Israel ambapo pia alizungumzia ujio wa waandishi wa habari kutoka nchini Israel ambao wanatembelea katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya ushirikiano wa kutangaza vivutio vya utalii baina ya Tanzania na Israel ambapo pia alizungumzia ujio wa waandishi wa habari kutoka nchini Israel ambao wanatembelea katika hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi./Picha: Mroki Mroki
*************
KATIKA kutangaza vivutio
vya utalii wa Tanzania kwa mataifa mengine, waandishi wa habari 10
wa vyombo mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamii na mawakala wa kampuni ya
usafirishaji kutoka Israel wamewasili
nchini kwa ziara ya siku tatu.
Katika ziara hiyo, ujumbe huo
utatembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko Kigoma ambayo ni maarufu kwa Sokwemtu, ikiwa ni mkakati wa kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika
Ukanda wa Kusini na Ukanda wa Magharibi.
Akizungumzia ujio huo leo Jijini
Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema ziara hiyo imeanza leo kwa watalii hao kuwasili na ndege yao moja kwa moja na kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume Kisiwani Zanzibar kisha kuruka tena hjadi Mkoani Kigoma na itamalizika Aprili 21,2017.
“Katika kutekeleza jukumu lake
kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani, Bodi ya Utalii tumekuwa
tukitumia mbinu mbalimbali kutangaza vivutio vilivyopo nchini,” alisema Jaji Mihayo.
Akazitaja baadhi ya mbinu zinazotumiwa na TTB kuwa ni pamoja
na kualika mawakala wa utalii, watu maarufu na waandishi wa habari kutoka nchi
mbalimbali duniani kutembelea Tanzania
na vivutio vyake ili wanaporudi kwao wavitangaze na kuwa mabalozi.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment