Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 30 March 2017

KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YAMWAGIZA MSAJILI HAZINA KUTAFUTA BODI YA TCAA



Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya  Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama amewaambia waandishi wa Habari Mjini Dodoma leo baada ya kumaliza kikao hicho kuwa, Kamati yake imepokea ripoti ya utendaji wa TCAA lakini wameshindwa kuijadili baada ya kubaini kuwa watendaji wakuu wote wa mamlaka hiyo hawapo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PIC, Albert Obama akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Lolencia Bukwimba na Katibu wa Kamati hiyo wakiendelea na kikao mjini Dodoma leo.
KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imegoma kujadili taarifa ya Malaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) hadi pale Msajili wa Hazina atakapo hakikisha kuwa Mamlaka hiyo inapata Bodi.


Mwenyekiti wa Kamati wa Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Albert Obama amewaambia waandishi wa Habari Mjini Dodoma leo baada ya kumaliza kikao hicho kuwa, Kamati yake imepokea ripoti ya utendaji wa TCAA lakini wameshindwa kuijadili baada ya kubaini kuwa watendaji wakuu wote wa mamlaka hiyo hawapo.



Obama alisema kuwa TCAA wametumwa wawakilishi tu, lakini kuanzia Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi wa Mamlaka ambao kimsingi ndio watendaji na ambao wanaidhinisha miradi hawapo.



“Kama Mkurugenzi wa TCAA na Mwenyekiti wa Bodi hakuweza kufika basi walau tungekuwa na  hata na Katibu Mkuu basi wa Wizara,” alisema Obama.



Alisema Kamati imemwagiza Msajili wa Hazina kwenda kuhakikisha uongozi wa Bodi na Menejimenti unakamilika ndipo wataomba kwa Spika wapangiwe kujieleza.



Kutokana na kushindikana kujieleza Kamati imeahirisha kuwapa nafasi kujieleza wajumbe watatu waliokuwapo ambao nao wana kaimu nafasi zao.



“Kamati hii ni mtambuka hivyo bila kuwapo waidhinishaji miradi na watekelezaji, ni vigumu kutoa maagizo kwa wajumbe badala ya viongozi,”alisema Obama.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment