Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen akingalia viroba vya unga wa sembe katika moja ya mashine za kusaga Unga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen
amesema kuwa Mkoa hauna njaa baada ya kufanya ziara katika maghala mbalimbali
ya wajasiriamali pamoja na kiwanda cha Unga cha Energy Mills vyote vilivyopo
katika mji wa Sumbawanga.
“Mmejionea wenyewe, Katika Manispaa ya Sumbawanga suala la
kwamba hakuna chakula ama kuna njaa ni maneno hewa, hakuna kitu kama hicho,
Chakula kipo cha kutosha nafaka karibu zote zipo,” Mkuu wa Mkoa alisisitiza.
Ameongeza kuwa wakulima wengi wameonekana kuuza mazo yao kwa
wachuuzi na kusababisha wafanyabiashara wa masokoni kwenda kununua mazao hayo
kwa bei na matokeo yake naoi li wapate faida nao wanaongeza bei jambo
linalosababisha wananchi kushindwa kununua na wao kulalamika kuwa hakuna wateja.
Katika suala la malalamiko ya wananchi kuosa pesa Zelote
Stephen alifafanua “malalamiko yaliyokuwepo kuwa pesa hakuna, nami nakubali,
kipindi hiki tulichopo ni wakati wa kilimo na wakati wa kilimo maana yake kila
mtu yupo shambani, na mwezi ujao (Februari) kuanzia tarehe 20, kuna taarifa
kwamba watu wataanza kuvuna maharage, kwahiyo ni dhahiri kwamba suala la njaa
na bei hakuna mtu ambae atalizungumzia.”
Katika kulishuhudia hilo mmiliki wa kiwanda cha Energy
Mills, Aziz Tawakali alisema kuwa mpaka sasa katika ghala lake ana tani 30 na
mifuko 3400 ya unga wa sembe wenye kilo 50 kwa kila mfuko, na kuongeza kuwa kwa
idadi hiyo kiwanda chake kinaweza kufanya biashara hadi mwezi wa tatu mwaka
huu.
“Sio kwamba kuna njaa, na katika mwaka mzima hatujawahi
kukosa stock ya chakula, na wa stock hii niliyonayo nina uwezo wa kuuza mpaka
mwezi wa tatu” Azizi alithibitisha.
Nae mmoja wa wamiliki wa mashine za mpunga Mathias James
amethibitisha kuwa katika Mkoa wa Rukwa hakuna shida ya chakula bali shida
iliyopo ni ya wateja wa kununua chakula hicho, hivyo aliwaasa wale wote
wanaosema kuwa hawana chakula cha kununua wafike katika ofisi yake.
“Kusema kuwa kuna njaa, hiyo si kweli, maana sisi
tunahangaika kutafuta wateja, na wateja tunaowategemea ni kutoka Mbeya na
Tunduma na wengine kutoka nchi za jirani kama Zambia na Kongo, hivyo tunawaasa
wale wanaotafuta mchele, kwetu upo, tuna magunia ya mpungaya kilo 90 zaidi ya
18,000 hayana wateja, mpunga upo, mahindi yapo, waohitaji watuone,” Mathias
alisisitiza.
Nao baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo wanouza kwa visado
nao pia waliendelea kulalamikia upungufu wa fedha katika mifuko yao na kuongeza
kuwa shida za wananchi si chakula kwa sasa bali pesa ndio ngumu na ndio
inayotusababishia njaa.
“Njaa yetu pesa hakuna chakula kipo ila hela ya kununulia hayo
mahindi ndio hakuna, kutokana na mzunguko wa biashara hela hakuna ila chakula
kipo,” Deus Malonga alisema.
Nae Agness Palakata alisema “Tokea asubuhi tunauza hilo
gunia halijaisha, sasa namna hii hatuwezi kurudi nyumbani uawalisha watoto,
pesa hakuna, chakula kipo ila pesa ndio tatizo, shida yetu na njaa yetu ni
pesa.”
Kwa kuthibitisha kutokuwepo kwa njaa Zelote Stephen aliongeza kuwa wakala wa taifa
wa hifadhi ya chakula (NFRA) wana jumla ya tani 15,500 ambazo zipo kwenye
magala yao.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment