Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji kutoka Hazina, Jones Mwalemba (kushoto) na Balozi Fouad Mustafa kutoka kampuni ya Albwardy
Investment Group wakikabidhiana hati ya Kiwanda cha Nyama Shinyanga. Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (aliyekaa keti) alishuhudia makabidhiano hayo
mjini Dodoma jana.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (mwenye miwani) akishuhudia
utiaji saini wa hati ya makabidhiano ya Kiwanda cha nyama cha Shinyanga.
Hati hiyo zilisainiwa na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji
Jones Mwalemba(aliyekaa upande wa kushoto) kutoka Hazina kwa upande wa
Serikali na Balozi Fouad Mustafa (aliyeinama upande wa kulia) kwa
upande wa Kampuni ya Albwardy Investment Group aliyemwakilisha mmiliki
wa Kampuni hiyo bwana Ali Saeed Juma Albwardy.
Hati
ya kiwanda cha nyama cha Shinyanga iliyorejeshwa Serikalini na Kampuni
ya Albwardy Investment Group baada ya kuuziwa kinyemela na kampuni ya
Tripple S Beef kinyume na mkataba iliyoingia na Serikali, baada ya
kampuni hiyo kushindwa kukiendesha kiwanda kwa miaka 11 tangu
kilipokabidhiwa.
Na John Mapepele, Dar es Salaam
Kampuni
ya Albwardy Investment Group imerejesha Serikalini hati ya kiwanda
cha nyama cha Shinyanga na eneo la kupumzishia mifugo la kiwanda hicho
iliyouziwa kinyemela na kampuni ya Triple S Beef Limited kutokana na
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kutoa siku saba kwa
wawekezaji Triple S Beef kusalimisha hati hizo kwa kushindwa
kukiendeleza kwa miaka 11.
Akizungumza mara baada ya kusaini
hati za makabidhiano ya hati hizo ofisini kwake jana, Waziri Mpina
alitoa siku 14 kwa Salim Said Seif ambaye ni mmiliki wa kampuni ya
Tripple S Beef kujisalimisha Serikalini kwa kuvunja mkataba na serikali
ambao ulimtaka kutommilikisha mwekezaji mwingine.
Hati hiyo
zilisainiwa na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji Jones
Mwalemba kutoka Hazina kwa upande wa Serikali na Balozi Fouad Mustafa
kwa upande wa Kampuni ya Albwardy Investment Group aliyemwakilisha
mmiliki wa Kampuni hiyo bwana Ali Saeed Juma Albwardy.
Waziri
Mpina alisema Kampuni ya Tripple S Beef ilinunua kiwanda hicho kwa
shilingi milioni 63 tu mwaka 2007 na kukiza kinyemela kwa shilingi
bilioni 8 kwa Kampuni ya Albwardy Investment Group mwaka 2015 kwa
mujibu wa maelezo ya mwakilishi wa kampuni hiyo, balozi Fouad Mustafa.
Aidha
alisema kiwanda hicho kilijengwa kwa bilioni 8.2 na kina ukubwa wa eneo
la hekta 32 huku likiwa na ziada ya eneo lenye hekta 444 zakuhifadhia
mifugo.
Aidha Mpina alisema mkakati wa Serikali kwa sasa ni
kuvifufua viwanda vyote vya nyama nchini na kuvitangaza kwa wawekezaji
makini ili waweze kuwekeza ili mifugo iliyopo iweze kupata soko la
uhakika na viwanda vilipe kodi za serikali hatimaye kuliingizia taifa
mapato.
“Tunaposema Serikali ya awamu hii ni ya viwanda tuna
maanisha kwa vitendo na kuhakikisha viwanda vyote vinafanya kazi katika
kiwango kinachositahili ili kujenga uchumi wa nchi yetu” alisistiza
Mpina
Aliongeza kuwakwa kuwa hati za kiwanda cha Shinyanga
zimekabidhiwa leo zabuni itatangazwa hivi karibuni ya kumpata mwekezaji
mahiri, pamoja na kiwanda hicho viwanda vingine vitakavyotangazwa kupata
mwekezaji mahiri ni pamoja na kiwanda cha nyama Mbeya na kiwanda cha
Ngozi cha Mwanza.
Alisema Serikali itavitangaza viwanda hivyo
pamoja kuvitengea maeneo makubwa ya kuhifadhia mifugo kabla ya
kuichinjwa ili kuinua ubora na thamani ya nyama katika masoko ya
kimataifa.
Akitoa taarifa ya Umilikishwaji wa kiwanda hicho,
Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji Jones Mwalemba kutoka
Hazina alisema kiwanda kilianza ujenzi wake mwaka 1975 na kwamba
kimegharimu dola za kimarekani milioni 3.5 na kilijengwa na Serikali
kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Alisema mwaka 2007 kiwanda hicho
kilibinafsishwa kwa mwekezaji Tripple S Beef Limited lakini kutoka na
matatizo ya uendeshaji kiwanda hicho kilifungwa mwaka 2017 na
kukabidhiwa kwa Serikali.
Awali Waziri Mpina alipofanya ziara
ya kushitukiza hivi karibuni katika kiwanda cha nyama cha Shinyanga
aliagiza kwamba ifikapo Juni 30 mwaka huu kiwanda hicho kiwe kimempata
mwekezaji ambaye ataanza kazi mara moja ya uchinjaji ili kutoa ajira
na kuliingizia taifa mapato.
Alitoa siku saba kwa wawekezaji
waliokuwa wanaendesha kiwanda hicho kusalimilisha hati za kiwanda na
eneo mara mmoja ili Serikali iweze kufanya taratibu za kufufua kiwanda
hicho.
Aidha amemuagiza Msajili wa Hazina kuanza uhakiki wa
mali zote za kiwanda hicho baada ya kubainika wizi uliokithiri katika
kiwanda hicho.
Pia Mpina ameamuru mmliki wa Kampuni inayolinda
kiwanda hicho kukamatwa mara moja na kufikishwa katika mikono ya sheria
kwa ajili ya kujibu mashitaka wa wizi wa mali za kiwanda hicho ambapo
alimtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuanzia sasa kiwanda hicho kilindwe
na vyombo vya Serikali badala ya makampuni binafsi.