Mhariri Mtemdaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara Simiyu lililofanyika Februari 13, 2017 katika Mji wa Bariadi mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na viongozi wote wa Mkoa wa Simiyu, wadau wa maendeleo na wafanyabiashara wa ndani na nje ya mkoa huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na kutoa pongezi kwa Kampuni ya Magazeti ya Serikali TSN kwa Jukwaa hilo la Biashara mkoani humo ambalo linatoa chachu ya kuhamasisha maendeleo mkoani humo.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato wa Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza na kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya kodi na kuahidi Mamlaka hiyo kufanya mchakato wa kufungua ofisi mkoani humu kuwapunguzia kero wafanyabiashara kulipa kodi
Washiriki ambao ni wafanya biashara kutoka ndani nanje ya mkoa wa Simiyu wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu.
******************
Na Mroki Mroki, TSN Digital-Simiyu
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) imejipanga kuitangaza Simiyu naTanzania kwa ujumla ndani na nje ya nchi.
Aidha TSN ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo inalenga na imejiandaa kutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu, kwa wadau mnalimbali nchini.
Akizungumza katika Jukwaa la Biashara Mkoani Simiyu, Mhariri Mtendaji wa TSN, Dkt Jim Yonazi alisema wakati umefika sasa wa jamii na wananchi kwa ujumla kuwa na mitizamo chanya, kwa kuziangalia changamoto kwa mtizamo wa kuzogeuza kuwa fursa.
Dkt Yonazi alisema umoja uwe ndio nguzo ya kutatua matatizo akitolea mfano wa Kobe na Sisimizi ambao walikuwa safarini lakini kobe alipopita njia akakuta mzoga wa tembo na kushindwa kupita na kurudi lakini Sisimizi walifika katika eneo la mzigo na ili kupata njia waliugeuza mzoga ule chakula (Fursa) walipoumaliza wakaendelea na safari na walipokutana na kobe aliwauliza ni vipi walifanikiwa kupita pale katika mzoga wa tembo na wakamjibu kuwa hawakuona mzoga wa tembo bali chakula.
Alisema wanasimiyu kamwe wasijione kuwa wapo katika mkoa mchanga ambao ni mkoa wa pembezoni mwa nchi lakini kama watatumia fursa zilizopo mkoani mwao basi watafanikiwa kuvuka na kusonga mbele na kuizidi mikoa iliyo endelea mapema.
"Tulipo amua kuja Simiyu kuendesha Jukwaa hili la Biashara wapo ambao walituambia kuwa kwanini mnaenda Simiyu ambayo ipo pembezoni, hakuna kitu cha maana huko, lakini sisi tuliona fursa na kuamua kuja kushirikiana nanyi kuziweka wazi fursa hizo," alisema Dkt Yonazi.
TSN iliratibu Jukwaa la Biashara Simiyu kwa kushirikiana
na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Benki ya NMB, Benki za TIB Development na
TIB Corporate na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Kutokana na majukumu yake, taasisi hizo ni muhimu
katika kusaidia uwekezaji Simiyu kufanyika kwa urahisi na hivyo kuleta tija kwa
wana-Simiyu na nchi kwa ujumla.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment