Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Kongamano la Mazingira
la Wanasayansi Watafiti wa bonde la Ziwa Victoria jijini Mwanza leo. Makamu wa Rais amewataka
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuibua
mbinu mpya zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazolikabili bonde la
Ziwa Victoria ikiwemo uchafu wa ziwa hilo unaotokana na shughuli za kibinadamu.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof Jumanne Makgembe akisalimiana na wadau mbalimbali wa Bonde la Ziwa Victoria akiwepo Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali, Dk Jim Yonazi (kulia kwa Waziri) nje ya ukumbi wa mkutano.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia Hotuba ya Makamu wa Rais.
Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo wa siku mbili na wameshiriki kikamilifu kw kuweka banda na watu mbalimbali wakiwepo viongozi wanalitembelea.
***************
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuibua
mbinu mpya zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazolikabili bonde la
Ziwa Victoria ikiwemo uchafu wa ziwa hilo unaotokana na shughuli za kibinadamu.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli
hiyo leo 15-Feb-2017 wakati
anafungua mkutano wa siku Mbili unaojuisha wadau wa mazingira, wasayansi na
watafiti wa bonde la Ziwa Victoria Jijini Mwanza.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni
chachu katika kuibua mbinu mpya na bora za kukabiliana na uharibifu wa
mazingira unaoendelea katika Bonde la Ziwa Victoria.
Amehimiza
kuwa kutokana na muhimu wa bonde hilo ni vyema wadau wote katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki kujumuika pamoja katika kulinda na kuendeleza uhifadhi wa
bonde hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa jumuiya hiyo.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema bonde la Ziwa Victoria bado linakabiliwa
na changamoto nyingi hasa kuibuka tena kwa magugumaji ambayo yameathiri shughuli
za uvuvi, usafiri na kuchafua maji katika Ziwa hilo hivyo ni muhimu kwa makundi
yote wakiwemo wanasayansi na watafiti kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto
hizo ambazo ni tishio kwa uhai wa Ziwa
Victoria.
“Kufanya Maamuzi kwa kuzingatia ushauri wa
kisayansi ni jambo zuri na la msingi katika kutunga sera ambazo zitasaidia kwa
kiasi kikubwa kulinda na kuhifadhi Bonde la Ziwa Victoria kwa ajili ya manufaa
ya wananchi wote”amesisitiza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza anaimani kubwa kuwa majadiliano
yatakayofanyika katika mkutano huo yatakuja na mbinu mpya ambazo zitatumika
katika kuhifadhi na kuendelea Bonde la Ziwa Victoria.
Katika
Mkutano huo wa siku Mbili unaofanyika Jijini Mwanza jumla ya mada 44
zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina na wadau wa mazingira, wanasayansi na
watafiti.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan pia alitembelea
mabanda mbalimbali ya maonyesho katika viwanja vya hoteli ya Malaika uliyopo
Jijini Mwanza.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment