Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa la Biashara jijini Mwanza hii leo Aprili 11,2017. Mongella katika hotuba yake alisema Mwanza inafursa mbalimbali za kiuchumi hivyo miaka michache ijayo anaamani kuwa Mwanza itashika usukani wa uchumi nchini na kuipiku Dar es Salaam.
Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim Yonazi akizungumza wakati wa Jukwaa la Biahara jijini Mwanza leo. TSN ndio waandaaji wa jukwaa hilo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Dk Yonazi amewaomba wadau mbali mbali
wamuunge mkono mkuu wa mkoa John Mongela katika juhudi za fursa za kibiashara na kuongeza kuwa TSN ni watu wa vitendo na
tunaendelea kutenda ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya kampuni hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi akizungumza katika Jukwaa la Biashara jijini Mwanza na mutoa Siri sita za kumsaidia mtu kufanikiwa katika biashara.
Meza kuu ikipiga picha na washariki wote.
Baadhi ya washiriki.
Na Alexander Sanga,Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela ameahidi
kuwa mkoa wake utakuja kuwa wa kwanza kitaifa katika kuwa na vitengo mbali
mbali vya uwekezaji.
Akizungumza katika jukwaa malumu la biashara
lilioandaliwa na kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Mongela alisema ni
wakati wa mkoa huo kubadilika na kuzitumia ipasavyo fursa za kibiashara kwa
manufaa ya sasa na badae.
Mongela alisema mkoa umetenga hekta 72 katika
eneo la Nyamongolo na hekta 500 katika eneo la Lwanyima kwajili ya ujenzi wa
viwanda kwa wadau watakaojitokeza katika uwekezaji huo.
Mkuu wa mkoa ameahidi kwa wadau watakaojitokeza
watapewa maeneo kwa kufuata taratibu za kisheria ndani ya wiki moja tu.
“Tunalenga kupata maeneo mengi zaidi kwa uwekezaji
na kurahisisha mchakato wa kuipata kwa ajili ya uwekezaji na mpaka sasa Pato la
Taifa(GDP) ya mkoa wetu sasa hivi ni shilingi
9.3trilion na tunaenda kwa kasi sana”Mongela alisema.
Mkuu wa mkoa alisema shilingi bilioni 7.6 zimetolewa kwa ajili ya mnara
wa kuongozea ndege ‘control tower’ itakayoonyesha mpaka Sudan kusini.
“Ndani ya miaka miwili Mwanza itapiga hatua
kubwa kwa miundombinu ya usafirishaji na viwanda vingi vinakuja na fursa kibao
za uwekezaji na endapo Stanadard Gauge ikikamilika mizigo ya Uganda itakuwa ikichukuliwa mkoani
kwetu” Mongela alisema.
Pia Mongela aliahidi endapo uwanja wa ndege wa
mkoani hapa ukikamilika ndege za kimataifa zitakuwa zikitua hapa.
Mkurugenzi mtendaji wa TSN, waandaaji wa Jukwaa
hilo la Biashara jijini Mwanza, Dr Jim Yonazi amewaomba wadau mbali mbali
wamuunge mkono mkuu wa mkoa John Mongela katika juhudi za fursa za kibiashara.
Dr Jim alisema kuwa TSN ni watu wa vitendo na
tunaendelea kutenda ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya kampuni hiyo.
“Mwanza itakuwa sehemu ya mikakati yetu na TSN
itaendlea kutoa huduma za kuwafikia wadau wote mkoani hapa” Yonazi alisema.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment