Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Dk Jim Yonazi akizungumza.
Dk Jim Yonazi alisema Jukwaa la Biashara ni
jambo kubwa, lenye kuleta faida nyingi kiuchumi, sio tu kwa mkoa wa Mwanza bali
kwa nchi nzima.
Alisema TSN imeamua kuitisha jukwaa hilo la
kiuchumi jijini Mwanza kwa kuwa mkoa wa Mwanza una utayari mkubwa katika kutumia
fursa za kiuchumi zilizopo kwa manufaa ya mkoa wenyewe na taifa kwa ujumla.
“Tuko
hapa kwa sababu sisi ni wapenda maendeleo na TSN tumeamua kuchagiza maendeleo
ya Mwanza,“ alisema.
Akiwasilisha salaamu za Waziri wa Habari,
Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk Hassan
Abbas alisema Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison
Mwakyembe amepongeza kuwepo kwa jukwaa hilo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya
nchi.
“Waziri
angetamani awe nasi hapa leo lakini kutokana na majukumu ya kitaifa, ameshindwa
kufika ila amesema ataendelea kuwa pamoja nasi kwa maamuzi yoyote
tutakayofikia,“ alisema.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan
Abbasi akizungumza katika Jukwaa la Biashara jijini Mwanza na mutoa Siri
sita za kumsaidia mtu kufanikiwa katika biashara.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi akitoa mada katika Jukwaa la Biashara jijini Mwanza.
Meza kuu na Washiriki wa Jukwaa la Biashara jijini Mwanza wakifuatilia mada ya fursa mbalimbali jijini Mwanza.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa wa NMB, Nsolo Mlozi, akitoa fursa za mitaji ambazo NMB Bank inawawezesha wafanya biashara wadogo na wakubwa nchini hivyo kuwataka wana Mwanza kujitokeza na kuchangamkia fursa hizo.
Wadau wa maendeleo kutoka jijini Mwanza wakifuatilia Jukwaa la Biashara jijini humo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
kurugenzi wa Mipango na masuala ya Ushirika wa TIB Development Bank, Patrick akizungumza ambapo alisema kuwa watu
wengi wana mawazo ya biashara lakini hawana miradi. Hivyo amewataka wana Mwanza kufika katika Bank za TIB ili mawazo yao yawezeshwe kuwa Biashara kwa kuwezesha kuwa na maandiko ya miradi na namna ya utekelezaji.
Mkurugenzi wa
TIB Corporate Bank, Frank Nyabundege yeye alisema TIB
raslimali kazi yake ni kubadilisha mawazo kuwa miradi. hivyo amewataka wana Mwanza
kuibua fursa.
"Tukiona linafaa tunawaambia wenzetu wa raslimali ambao
wanaliangalia kama linafaa kuwa bankable. Ukienda development, unapewa pesa ya
kunenga kiwanda, na working capital unakuja kwetu, nchi
yetu inapokwenda kwenye uchumi wa viwanda basi benki inayowafaa ni TIB," alisema Nyabundege.
Mkuu wa Mkowa wa Mwanza, John Mongella akizungumza na kueleza yale yaliyopo ndani ya Mkoa wa Mwanza na namna ambavyo wanaweza kuwahudumia wawekezaji.
“Hatuko tena kwenye mikakati. Tumeshaanza na
hivyo tunataka muitazame Mwanza kwa jicho tofauti,“ alisema.
Alisema katika kuweka mazingira mazuri kwa
wawekezaji na kuondoa changamoto zinazowakabili, mkoa umeunda kitengo maalumu
cha kushughulikia masuala ya uwekezaji na biashara.
“Tunataka Mwekezaji kama ana mgogoro na TRA,
kitengo hiki kiende naye moja kwa moja TRA ili wamsaidie, wakajadiliane naye,“
alisema huku akifafanua kwamba kabla ya kuundwa kwa kitengo hicho kulikuwa na
malalamiko mbalimbali ya wawekezaji mkoani mwake.
“Bila
shaka sisi Mwanza ndio wa kwanza kuanzisha kitengo cha uwekezaji ingawa hakiko
katika taratibu zetu za kiserikali. Kinajumuisha wahandisi, wachumi,
watengeneza mipango na kadhalika,” alisema.
Mkurugenzi wa DTBi, George Mulamula akizungumza katika Jukwaa la Biashara jijini Mwanza.
Jukwaa la biashara ambalo jana lilihudhuriwa
na watu zaidi 300 liliwashirikisha pia wadau wa maendeleo ambao pia
wamelidhamini.
Baadhi ya wadau walitoa elimu muhimu kwa
wafanyabiashara wa Mwanza ni pamoja na mabenki ya NMB, TIB (Development), TIB
(Corporate) na Benki ya Posta (TPB). Taasisi hizi za fedha zilieleza, pamoja na
mambo mengine, namna wafanyabiashara wanavyoweza kupata fedha za mitaji
alimradi waweze kutekeleza masharti fulani fulani.
Wadau wengine waliotoa mada zao jana ni Kampuni ya Simu ya nchini (TTCL), Mfuko wa Bima ya
Afya (NHIF) kampuni ya simu ya Vodacom na hoteli ya kisasa jijini Mwanza ya Victoria Palace.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment