Mku wa
Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akizungumza na katika kikao kazi cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu
za serikali(CAG) kwa mwaka 2015/16 na kuzitaka Halmashauri za wilaya
Mkoani Mbeya kufanya kazi kwa uadilifu na umakini kuhakikisha wanapata hati
safi.
Washiriki wakichangia maoni yao.
MKUU wa Mkoa
wa Mbeya, Amos Makalla amezikata Halmashauri za wilaya Mkoani Mbeya kufanya
kazi kwa uadilifu na umakini kuhakikisha wanapata hati safi.
Makalla aliyasema hay oleo wakati akiongoza kikao cha kujadili taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali(CAG) kwa mwaka 2015/16.
katika taarifa hiyo ya CAG kati ya Halmashauri saba za Mkoa wa Mbeya sita zimepata hati inayoridhisha na moja imepata hati ya mashaka.
Ameagiza taarifa hiyo ijadiliwe kwenye ngazi ya Menejiment, Kamati za Fedha na mipango na Baraza la madiwani.
Pia ameagiza hoja zote zilizoibuliwa na CAG za mwaka 205/16 na miaka ya nyuma zipatiwe majibu.
Amesema taarifa za wakaguzi wa ndani
zifanyiwe kazi kwani kupuuza hoja za wakaguzi wa ndani ndiyo chanzo cha kupata
hati chafu.
Kikao hicho pia kimeweka maazimio 20 ya kuhakikisha Halmashauri zinapata hati safi, uboreshaji wa mapato, kudhibiti upotevu wa mapato,kuepuka mikataba mibovu , usimamizi wa miradi na tija na kutenga fedha kwa ajili ya mikopo ya vijana na wanawake.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment