Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mama Janeth Magufuli na Mama Mwanamema Shein kwenye sherehe hizo
Viongozi mbalimbali katika Jukwaa kuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe
za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
leo Desemba 9, 2017
Viongozi mbalimbali katika Jukwaa kuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe
za kuadhimisha miaka 56 ya Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
leo Desemba 9, 2017
Marais Wastaafu Mhe Benjamin Mkapa na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete wakiteta
jambo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu
Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya
Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017
Gwaride lililoundwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama vikipita
mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu
Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya
Uhuru katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo Desemba 9, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09
Desemba, 2017 amewaongoza Watanzania kusherehekea maadhimisho ya miaka 56 ya
Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Sherehe
hizo zimehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Spika wa Baraza la Wawakilishi
Mhe. Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika
wa Bunge wa Bunge la Morocco Mhe. Hakim Benchamach, Marais wastaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine wastaafu na wanaoongoza taasisi
mbalimbali.
Pamoja
na kukagua gwaride rasmi na kupigiwa mizinga 21 kwa heshima yake, Mhe. Rais
Magufuli, viongozi mbalimbali na wananchi wameshuhudia maonesho mbalimbali
yaliyofanywa na kikundi cha komandoo, askari wa kupambana na ugaidi, ndege za
kivita, gwaride la wanafunzi, ngoma za asili, kwaya na muziki wa wasanii wa
kizazi kipya (Bongo Fleva) walioimba
wimbo maalum wa uzalendo kwa Tanzania.
Akizungumza
katika sherehe hizo Mhe. Rais Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8,157 ambao
ni sehemu ya wafungwa wote 39,000 waliopo magerezani wakitumikia vifungo
mbalimbali.
Kati
ya wafungwa hao, 6,329 wamepunguziwa adhabu na 1,828 wameachiwa huru kuanzia
leo wakiwemo 61 waliohukumiwa kunyongwa na waliokuwa wakitumikia vifungo vya
maisha, na amewataja miongoni mwao kuwa ni Mganga Matonya aliyefungwa gerezani
kwa miaka 44 na mwenye umri wa miaka 85, wanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanae Johnson Nguza (Papii Kocha)
“Nawapa
msamaha wafungwa hawa kwa mujibu wa ibara ya 45 ibara ndogo ya 1 ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayonipa mamlaka hayo, nimeamua kufanya hivi
kwa sababu baadhi ya wafungwa wanaotumikia vifungo vya maisha ni wazee sana na
wangine wameonesha mwenendo mzuri wa kitabia wakiwa gerezani”
“Na
hawa niliowapa msamaha sio wale waliojihusisha na mauaji ya watu wenye ualbino
na waliofungwa kwa kuhusika katika ujambazi” amesema
Mhe. Rais Magufuli.
Hata
hivyo Mhe. Rais Magufuli ameonya kuwa msahama alioutoa usitafsiriwe kwa
kuhalalisha watu kujihusisha katika uhalifu na amesisitiza kuwa vyombo vya dola
vitaendelea kusimamia sheria.
Mhe.
Rais Magufuli amewapongeza Watanzania wote kwa kufikisha miaka 56 ya Uhuru na
kubainisha kuwa katika kipindi hicho nchi imepiga hatua kubwa katika maendeleo
ikiwemo kuongezeka mtandao wa barabara kutoka kilometa 33,600 hadi kufikia
kilometa 150,946, kati yake kilometa za lami zikiwa zimeongezeka kutoka 1,360
hadi 12,679.55.
Aidha,
ameongeza kuwa Wakala wa barabara nchini (TANROADS)
inaendelea na ujenzi wa barabara nyingine za lami zenye kilometa 2,480 na
barabara nyingine za lami zenye urefu wa kilometa 7,087 zipo katika maandalizi
ya kuanza ujenzi.
Maeneo
mengine ambayo Tanzania imepiga hatua ni kuongezeka kwa shule za msingi kutoka
3,100 hadi 17,379, shule za sekondari kutoka 41 hadi 4,817, vyuo vikuu kutoka 1
hadi 48, Madaktari waliosajiliwa kutoka 403 hadi 9,343, Wahandisi waliosajiliwa
kutoka 2 hadi 19,164 na Wakandarasi kutoka 2 hadi 9,350.
“Kwa
hiyo ndugu zangu tumepiga hatua kubwa sana, hata wastani wa maisha yetu
umepanda kutoka miaka 37 hadi 61 na pia idadi yetu imeongeza kutoka watu
Milioni 9 hadi Milioni 52” amesisitiza Mhe.
Rais Magufuli.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment