Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Sunday, 10 December 2017

MBUNGE WA ZAMANI WA SINGIDA KUSINI AFARIKI DUNIA

MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga (72) afariki dunia.

Daily News Digital Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Siginda, Martha Mlata amethibitisha juu ya kifo hicho na kusema kuwa bado anafanya mawasiliano na familia ya marehemu kujua taratibu zaidi.Anaandika Mroki Mroki, Dodoma.

"Nikweli tumempoteza ndugu yetu, Mohamedi Misanga alfajiri ya leo katika Hospitali ya Muhimbili ambako taarifa za awali zinasema kuwa jana alipatwa na tatizo akapelekwa hospitalini hapo kwa matibabu na bahati mbaya leo amepoteza maisha," alisema Mlata.

Misanga aliyezaliwa Marchi 15, 1945, amepata kuwa Mbunge katika jimbo hilo kwa vipindi vitatu toka mwaka 2000-2015 amefikwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Ndani ya Bunge amewahi kuongoza na kuwa mjumbe wa Kamati mbalimbali za Kudumu za Bunge hususani ile ya Miundombinu.

Aidha Misanga pia amepata kushika nyadhifa mbalimbali katika vyama vya Michezo hasa vya Mpira wa Miguu kwani aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) hivi sasa TFF na baade kuwa mjumbe katika kamati mbalimbali za TFF huku akiwa ni mnzi mkubwa wa Klabu ya Soka ya Yanga ya Dar es Salaam.

Aidha msiba kwa sasa upo nyumbani kwake Morocco jijini Dar es Salaam jirani na jengo la Airtel ambapo mwili unataraji kusafirishwa kesho kwenda kijijini kwake mkoani Singida kwa maziko.

Endelea kuwa nasi Daily News Digital kwa taarifa zaidi.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment