Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla au Chief Mwaigonela wa Iduda akizungumza na wananchi wa Kata ya Iduda jijini Mbeya katika moja ya mikutano yake kusikiliza kero za wananchi.
Makalla aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara katika Kata ya Iduda jijini Mbeya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbali na kusikiliza kero hizo katika utaratibu wake aliyojiwekea wa kusikiliza kero hizo mara mbili kwa mwezi, Makalla alichangia ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Iduda kwa kutoa mifuko 100 ya saruji na kulitaka jiji kuunga mkono.
Ameagiza pia eneo hilo la kituo cha Afya kujengwa uzio ili kuzuia wavamizi wa maeneo.
Aidha kwa upande wao wananchi wa Iduda wameitaka Malka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi ya majengo kuwaepusha na usumbufu.
Kutokana na utendaji wake wa kazi tangubaingie mkoa wa Mbeya, wananchi wa mkoa huo na wazee wa Kata ya Iduda wamemsimika rasmi kua Chief wa Iduda kwa jina la Mwaigonela.
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla akikagua ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Iduda.
Amosn Makalla akisimikwa na wazee wa Kata ya Iduda kuwa Chief wa Iduda
****************
MKUU wa Mkoa wa Mbeya' Amos Makalla amewataka wananchi na wakazi wa mkoa huo kujijengea tabia ya kuchangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao.Makalla aliyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara katika Kata ya Iduda jijini Mbeya kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbali na kusikiliza kero hizo katika utaratibu wake aliyojiwekea wa kusikiliza kero hizo mara mbili kwa mwezi, Makalla alichangia ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata ya Iduda kwa kutoa mifuko 100 ya saruji na kulitaka jiji kuunga mkono.
Ameagiza pia eneo hilo la kituo cha Afya kujengwa uzio ili kuzuia wavamizi wa maeneo.
Aidha kwa upande wao wananchi wa Iduda wameitaka Malka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi ya majengo kuwaepusha na usumbufu.
Kutokana na utendaji wake wa kazi tangubaingie mkoa wa Mbeya, wananchi wa mkoa huo na wazee wa Kata ya Iduda wamemsimika rasmi kua Chief wa Iduda kwa jina la Mwaigonela.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment