Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Agustine Mahiga akifurahi na Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa, Maite Nkoana-Mashabane wakati wa Kikao cha Tume ya Ushirikiano wa Marais (BNC) ngazi ya Mawaziri.
*********
Rais John Magufuli,na Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma kesho wanatarajiwa kushuhudia utiliwaji saini wa Mikataba ya Makubaliano (MoU) katika maeneo makuu mawili.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Agustine Mahiga, maeneo hayo yanayotarajiwa kutiliwa saini ni sekta ya uchukuzi na uhifadhi.
Dk Mhiga ameyasema hayo leo baada ya kumalizika kwa kikao cha Tume ya Ushirikiano wa Marais (BNC) ngazi ya Mawaziri wa Tanzania na Afrika Kusini ambapo kwa upande wa Afrika Kusini mawaziri hao waliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikianobwa Kimataifa, Maite Nkoana - Mashabane.

Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment