Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Monday, 22 May 2017

MKUU WA MKOA AWAAGIZA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI KUFANYA KAZI KWA KARIBU NA VIONGOZI WA USHIRIKA

MKUU wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewaagiza Wakuu wa Wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri ndani ya Mkoa wa Mbeya kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa Ushirika.

Makalla ameyasema hayo leo wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vyama vya msingi wa zao la Tumbaku Wilaya ya Chunya.

Makalla amesema hatua hiyo ni katika kukabiliana na changamoto za Pembejeo, Masoko na Bei za bidhaa au mazao.

Amesema lengo la serikali ni kuwa na ushirika wenye nguvu na unaochangia kujenga uchumi.

Makalla amesema ushirika unakufa pale unapoendeshwa bila kufuata taratibu na sheria,ushirika usiokaguliwa hesabu zake , ushirika usiyo na mikutano na wanachama wake.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment