Jengo la Rock City Mall ambako Jukwaa la Biashara jijini Mwanza linatafanyika hapo kesho Aprili 11,2017.
Mandhari za jiji la Mwanza
Na Mroki Mroki, Mwanza
ZAIDI ya watu 300 wanataraji kushiriki katika Jukwaa la Biashara jijini mwanza ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza na Daily News-Habarileo Blog, Mkuu wa mkoa Mwanza, John Mongella, amewataka wote
waliopata mwaliko kuhakikisha wanahudhuria kwenye jukwaa hilo bila kukosa ili
kufaidika na mada motomoto zitakazotolewa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Jukwaa hilo litafanyika katika ukumbi wa Rock City Mall, moja ya majengo nadhifu na
kivutio kikubwa jijini Mwanza.
Miongoni mwa watoa mada katika Jukwaa hilo ambalo pia litahudhuriwa na Waziri wa habari, Utamaduni sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali
(TSN), inayochapisha magazeti ya HabariLeo,
Daily News na SpotiLeo, Dk Jim Yonazi.
Miongoni mwa washiriki katika Jukwaa hilo la aina yake ambalo litakuwa likibainisha fursa mbalimbali zilizopo mkoani Mwanza ni pamoja na wafanyabiashara
wadogo wakiwemo madereva wa bodaboda, teksi na daladala.
Pia kutakuwa na wauza
bidhaa kwenye masoko mbalimbali mkoani Mwanza, wauza mitumba na wauza samaki na
dagaa.
Nae Mhandisi
Bonface Nyambele anayeratibu Jukwaa hilo kwa upande wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na
Patrice Simbachawane wa TSN, wengine walioalikwa ni wafanyabiashara wa kubwa na
wakati, wafanyabisahara wanawake na wamiliki wa viwanda na Hoteli mbalimbali za kitalii zilizopo jijini Mwanza.
Mkoa wa Mwanza una
viwanda 86 kwa mujibu wa Kitengo cha Uwekezaji mkoani Mwanza kinachoongozwa na
Mhandisi Nyambele sambamba na maofisa wengine waandamizi sita.
Aidha TSN imeandaa toleo maalum la habari mbalimbali za fursa na maendeleo ambalo litachapishwa katika gazeti la Habarileo Aprili 11,2017, lakini taarifa za jukwaa hilo zitarushwa hewani mbashara katika mitandao ya kijamii ya facebook, Twitter, Instagram na youtube.
Baadhi ya wadau wa maendeleo
waliothibitisha kutoa elimu adhimu na muhimu kwa maendeleo ya Mwanza ni pamoja
na Kampuni
ya Simu ya nchini (TTCL), Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kampuni ya simu ya
Vodacom, hoteli ya kisasa jijini Mwanza ya Victoria Palace na Mfuko wa Pensheni
wa PPF.
Wadau wengine ni benki za NMB, TIB
(Development), TIB (Corporate) na Benki ya Posta (TPB).
Wengine ni Mamlaka ya Mapato (TRA), Baraza la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF), Watumishi Housing Company (WHC) Ariel Glaser Pediatric
Aids Healthcare Initiative (AGPAHI), Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Baraza la
Biashara Tanzania.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment