Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akikagua kiwanda cha kuchinja
Punda cha Hua Cheng Limited
kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma
alichokifungua hivi karibuni leo.
(Picha na Jumanne Mnyau)
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akipokea maelezo ya usindikaji
wa nyama Punda kutoka kwa mfanyakazi wa wa kiwanda cha kuchinja
Punda cha Hua Cheng Limited
Elizabeth Peter.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani) akitembezwa katika kiwanda
cha kuchinja Punda
cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni na Meneja Mkuu wa kiwanda hicho
bwana Xun Long Go
****************************
Na John Mapepele, Dodoma
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amewataka wawekezaji wa viwanda vya kuchinja
Punda nchini kupandisha bei ya kununua wanyama hao badala ya shilingi laki
mbili ya sasa kwa punda mmoja ili kudhibiti utoroshaji wa mifugo
nje ya nchi ambapo inakadiriwa kuwa
zaidi ya mifugo elfu kumi
inatoroshwa mipakani kwa siku kwenda nje
ya nchi inakonunuliwa kwa bei ya juu.
Akizungumza leo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika
Kiwanda cha Punda cha Hua Cheng Limited kilichopo nje kidogo ya
mji wa Dodoma alichokifungua hivi karibuni, Waziri Mpina alisema bei hiyo haiendani na gharama halisi ya ufugaji wa Punda haliinayowafanya wafugaji kuwatorosha mifugo na
kulikosesha taifa mapato makubwa.
Alisema ili punda aweze kufikia hatua ya kuchinjwa inachukua
kiasi cha miaka miwili ambapo gharama zake za ufugaji zinakuwa
juu ukilinganisha na bei ya shilingi laki mbili anayouzwa kwa wenye viwanda vya punda nchini.
Aidha alisema kumekuwa
na utoroshaji mkubwa wa
mifugo wanaokadiriwa kufikia
takribani 1,614,035 kwa mwaka unaofanyika
kwenye mipaka ya nchi yetu ambapo
takribani shilingi bilioni 32.28 zinapotea kama ushuru na takribani shilingi bilioni 24.21 zinapotea
kutokana na kodi ya mapato ambayo ingelipwa kwa nyama ambayo ingeuzwa hapo nchini.
Aidha Mpina
ameunda tume ya wataalam kutoka
Wizarani kwa ajili ya kuja kufanya
tathmini kama kiwanda hicho kimetimiza
masharti yote yaliyotolewa na Serikali
baada ya kukifungua Februari mosi
mwaka huu ambapo alisema ikibainika
kuwa kiwanda hakijakidhi masharti yaliyotolewa na Serikali kitachukuliwa hatua kali zaidi za kisheria
ikiwa ni pamoja na kukifungia kufanya
kazi zake.
Aliyataja baadhi ya masharti
yaliyotolewa na Serikali wakati wa kukifunga kiwanda hicho Julai 2017
kuwa ni pamoja na kuwa na ranchi za punda, kuboresha kosaafu za Punda nchini, kuunda na kuingia mikataba
na vikundi vya wafugaji wa Punda na kuwa na Punda wasiopungua mia tatu katika eneo la
kuhifadhia mifugo kabla ya kuchinjwa ili
kuwa kuhakikisha kwamba mifugo
wanaangaliwa kwa wiki mbili kabla ya kuchinjwa
ili wawe katika ubora wa kimataifa.
Waziri Mpina alisema
uwekezaji wa aina hiyo wa kuongeza thamani ya mazao ya mifugo ni moja ya
vipaumbele vya wizara yake kwa sasa ili kuchochea kwa kasi kufanikisha azma ya
Tanzania ya viwanda.
Aidha aliwahakikishia
wawekezaji wa kiwanda hicho kuwa
endapo watakuwa wamekamilisha masharti atawapa kibali cha kudumu ambapo pia
atawaongezea idadi ya kuchinja Punda
kutoka punda 20 wa sasa ili vijana
wengi wapate ajira na kiwanda kiweze
kuchangia zaidi katika mapato ya
Serikali.
Mpina aliwahimiza wawekezaji hao kuhakikisha
wanawasaidia wafugaji katika kuongeza
uzalishaji, kupambana na maradhi,
upatikanaji wa maji na malisho kwa mifugo.
Alisema idadi ya punda waliopo nchini ni 520,000 tu hivyo
juhudi za makusudi zinahitajika kuongeza uzalishaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Xun Long Go
alimshukuru Waziri Mpina kwa kufungua
kiwanda hicho ambapo amesema hadi sasa
kiwanda kimezalisha na kuuza
tani 224 za nyama ya Punda kwenda nchini China na Vietinam
ambapo pia tani 52 za ngozi ya
Punda ilizalishwa na kuuzwa kuanzi mwezi
Februari, 2018.
Alisema kiwanda hicho kimeajiri watanzania 55 ambapo hadi
sasa kina punda 88 katika maeneo ya Chalinze na Zuzu mkoani Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa
Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Lucia
Chacha aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kwa kubuni mbinu za
kuwasaidia wafugaji kwa kuwapatia elimu
bora zaidi ya ufufaji wa punda ili waweze kuwazalisha kwa wingi zaidi kuliko ilivyo sasa
Hivi sasa Tanzania ina viwanda viwili tu vya kuchinja na
kuuza nyama ya punda ambavyo ni kiwanda
cha Punda cha Huacheng Limited kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma na Kiwanda
cha Fang Hua kilichopo Shinyanga ambavyo vyote
vimepewa kibali cha kuchinja Punda 20 kwa siku kila kimoja.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment