Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina(Mwenye
Miwani) akioneshwa eneo la kiwanda cha
nyama Shinyanga na Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji kutoka Ofisi
ya Msajili wa Hazina Jones Mwalemba(aliyenyoosha mkono) Kushoto kwake ni
Mkurugenzi wa Uzalishaji Mifugo na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Asimwe Lovince kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Wilaya a shinyanga wa CCM.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi
Luhaga ( Mwenye Miwani) Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Shinyanga Abubakari Mkadamu akivunja kufuli la mlango mkuu wa
kuingilia katika kiwanda cha nyama
Shinyanga mara baada ya waziri Mpina kufanya ziara ya
kushitukiza katika kiwanda hicho. (Picha na John Mapepele)
**********************
Na
John Mapepele, Shinyanga
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina
ametoa siku saba kwa wawekezaji
wa kiwanda cha nyama Shinyanga cha Kampuni ya Triple S Beef Limited na Agri
Vision kuwasilisha hati zote
za umiliki hati ya eneo la kiwanda na eneo la kuhifadhia mifugo baadha ya kushindwa kukiendeleza kwa miaka 11.
Akizungumza
katika kiwanda hicho leo Mpina amuagiza Mkurugenzi wa Ubinafsishaji na Ufuatiliaji Jones Mwalemba kutoka Hazina kuhakikisha kwamba
ifikapo Juni 30 mwaka huu kiwanda hicho kiwe kimempata mwekezaji ambaye ataanza kazi mara moja ya
uchinjaji ili kutoa ajira na kuliingizia
taifa mapato.
Aidha
amemuagiza Msajili wa Hazina kuanza uhakiki wa mali zote za kiwanda hicho
baada ya kubainika wizi uliokithiri
katika kiwanda hicho.
Pia
Mpina ameamuru mmliki wa Kampuni inayolinda kiwanda hicho kukamatwa
mara moja na kufikishwa katika mikono ya sheria kwa ajili ya kujibu mashitaka wa wizi wa mali za kiwanda hicho ambapo amemtaka Mkuu wa Mkoa kuhakikisha kuanzia sasa kiwanda hicho
kilindwe na vyombo vya Serikali badala ya makampuni binafsi.
Waziri
Mpina alisema hatua ya Kampuni ya Triple S kuuza kiwanda na kuingia mkataba mpya na Kampuni
ya Agrovisioni ni kinyume na
mkataba wa awali ilioingia na Serikali.
“Huu
ni ukiukwaji wa masharti ya Mkataba
kulingana na kifungo cha 16.1
ambapo sasa kinauondoa umiliki wake
katika kiwanda hiki” alisisitiza Mpina
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Masoko wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Lovince Asimwe kiwanda kilianza ujenzi wake mwaka 1975 na
kwamba kimegharimu dola za kimarekani
milioni tatu na kilijengwa na Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.
Alisema
mwaka 2007 kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa mwekezaji Tripple S Beef Limited lakini kutoka na na matatizo ya uendeshaji
kiwanda hicho kilifungwa mwaka 2017 na kukabidhiwa kwa Serikali.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment