Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 6 December 2017

TIB CORPORATE BANK WAIPIGA TAFU ZAHANATI YA MSONGOLA DAR ES SALAAM

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Edward Lyimo (wa tatu kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya tiba ya uzazi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kwa ajili ya Zahanati ya Msongola nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo. Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 7 vitasaidia kupunguza mahitaji ya vifaa tiba kwa wodi ya wazazi ya zahanati hiyo inayohudumia wanawake wazazi Zaidi ya 50 kwa mwezi. Pamoja nao (kutoka kushoto) ni Mkurugenzi wa Huduma za matawi na Masoko, Theresia Soka, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Chacha Mwita, Mkurugenzi wa hazina Bahati Minja, Mkurugenzi wa mikopo, Adolphina William na maafisa wengine wa benki na hospitali hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Edward Lyimo (wa pili kushoto) akimpatia maelezo mafupi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhusu sehemu ya vifaa vya tiba ya uzazi benki hiyo ilivyotoa kwa ajili ya Zahanati ya Msongola nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam leo kabla ya makabidhiano. Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Dkt Mwanahawa Malika. 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akiongea na wana habari wakati wa hafla hiyo ya kupokea msaada wa vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 7 vitakavyosaidia kupunguza mahitaji ya vifaa tiba kwa wodi ya wazazi ya zahanati hiyo inayohudumia wanawake wazazi Zaidi ya 50 kwa mwezi. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIB Corporate Bank, Edward Lyimo (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa hafla hiyo. (Picha na Robert Okanda Blogs) Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment