Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Nafasi Ya Matangazo

Wednesday, 24 May 2017

RAIS MAGUFULI ATENGUA RASMI UTEUZI WA WAZIRI WA NISHATI NA MADINIRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo kuanzia leo tarehe 24 Mei, 2017.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.

Kutenguliwa kwa Prof Muhongo kumekuja saa chache baada ya Rais Magufuli kupokea taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Mara baada ya kupokea ripoti hiyo Rais Magufuli alitangaza maamuzi mbalimbali aliyoyachukua kutokana na taarifa hiyo ikiwa ni pamoja na kuvunja bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMMA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi mkuu wa TMMA ikiwa ni mapendekezo ya Kamati hiyo. 

Hii ni mara ya pili kwa Prof Sospeter Muhongo kuondolewa katika Wizara hiyo, baada ya Januari 24,2015 alipojiuzulu kufuatia shinikizo baada ya kashfa ya Escrow, na Rais Magufuli alipoingia madarakani alimrejesha katika wadhifa huo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment