Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday, 15 April 2017

VIVUTIO VYA TANZANIA NA BODI YA UTALII VYAINGIZWA KATIKA KUWANIA TUZO ZA DUNIA

 Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.
 Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Mlima Kilimnajaro na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) vimeingizwa katika kinyang’anyiro cha akuwania tuzo za 24 za utalii Duniani (World Travel Awards) katika tukio la utoaji tuzo hizo litakalo fanyika Kigali Rwanda katyika hoteli  ya Radison Blu tarehe 11 Oktoba 2017 ambapo washindi  katikamakundi mbalimbnali watakabidhiwa tuzo.

Katika shindano hilo la kuwania tuzo mbalimbali kwa mwaka huu wa 2017, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti  itapambana na hifadhi nyingine barani Barani Afrika kama vile Central Kalahari Game Reserve ya Bostwana, Etosha National Park (ya Namibia, Kidepo Valley National Park ya Uganda, Kruger National Park ya Afrika Kusini, na  Masai National Reseve ya Kenya, katika kundi la ‘Hifadhi ya Taifa inayoongoza Barani Agrka kwa mwaka 2017’.

Vivutio kingine cha utalii kutoka Tanzania kilichoingia katika shindano hilo vikishindana katika kundi la ‘Kivutio kinachoongoza Barani Afrika 2017’ ni Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko barani Afrika, na bonde la Ngorongoro ambalo pia ni maajabu ya nane ya dunia. Vivutio hivi  vinashindana na vivutio vingine kama Mapiramidi ya Giza kutoka Misri, Kisiwa cha Robben cha Afrka Kusini, Mlima wa Meza (Table Mountain) wa Afrika Kusini, na V&A Waterfront kutoka Afrika Kusini.

Aidha Bodfi ya Utalii Tanzania (TTB) ambayo ni Shirika la Umma lenye dhamana ya kuitangza Tanzania kama eneo bora la utalii Duniani imefuzu katika kuwania tuzo ya ‘Bodi ya Utalii inayoongoza Barani Afrika kwa mwaka 2017’ ikichuana na Bodi za Utalii kutoka nchi nyingine Afrika kama vile Misri, Gambia, Ghana, Kenya na Morocco. Nchi nyingine ni Namibia, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini na Zanzibar.

Katika shindalo la mwaka jana 2016 la kuwania tuzo hizo za Dunia Mlima Kilimanjaro uliibuka mshindi na kukabidhiwa tuzo ya ushindi wa kwanza kwa kuwa Kivutio kinachoongoza barani Afrika kikivipiga kumbo vivutio vingine katika kundi la ‘Kivutio kinachoongoza Barani Afrika’.

Namna ya kupiga kura:
Ili uweze kupiaga kura unatakiwa kwanza ujisajiri na kufungua akaunti. Ili kujisajili na hatimaye kupiga kura yako tafadhali tembelea tovuti ifuatayo: 

www.worldtravelawards.com/register. Mara baada ya kujisajili na kufungua akaunti utaletewa barua pepe kupitia akaunti yako hiyo na hapo utautatakiwa kugonga kwenye kiunganishi cha uthibitisho ili kuthibitisha anuani ya barua pepe yako kabla ya kuingia na kupiga kura yako. Zoezi la kupiga kura liko wazi na litaendelea mpaka Agosti 21, 2017.
Bodi ya Utalii Tanzania inatoa wito kwa watanzania kujisali kupitia tovuti hiyo na kuvipigia kura vivutio vyetu vyote vya utalii katika shindano hilo pamoja na Bodi yetu ya Utalii Tanzania (TTB).


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment