Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama
akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke alipomtembelea
waziri Ofisini kwake Bungeni Dodoma.
Na Mwandishi Wetu
Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania, Sarah Cooke amesema nchi yake ipo tayari kuisaidia Tanzania katika
kutoa mafunzo maalum ya Menejimenti ya Maafa kwa wataalamu wetu.
Ameyasema hayo hivi karibuni
wakati alipomtembelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira
na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ofisini kwake mjini Dodoma.
Akielezea lengo la ziara hiyo,
Balozi Cooke alisema Serikali yake inataka kuiunga mkono Serikali ya Tanzania
katika kuhakikisha inajipanga kukabili na kurejesha hali pindi yanapotokea maafa.
“Masuala ya maafa yapo nchi nyingi ikiwemo
kwetu Uingereza ingawa mafuriko na ajali za moto zimekuwa zikiikumbaa nchi yetu
mara kadhaa.”Alisema Balozi.
Aliongeza kuwa, Serikali ya Uingereza imevutiwa na juhudi zinazofanywa na Serikali
ya Tanzania katika kukabili na kurejesha hali ikiwa pamoja na kuwasaidia wananchi na mali zao pindi
yanapotokea maafa.
Kwa upande wake, Waziri Mhagama
alimpongeza Balozi huyo kuona umuhimu wa kuja Tanzania na kuonesha nia ya kuisaidia
nchi kwa namna mbalimbali.
“Nishukuru kipekee kwa ujio
wako na kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika
maswala mazima ya maafa na kumhakikishia kuwa Tanzania ipo tayari na itajiandaa
kuwaunga mkono kwa utayari wa kuisaidia nchi”Alisema waziri Mhagama.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment