JAMII imetakiwa kupiga
vita vitendo vya ukatili wa kijinsia watoto na wazee ikiwa na pamoja na
viongozi wa dini kuzitumia nafasi zao kukomesha ukatili huo.
Akifungua katika mkutano wa wadau uliowashirikisha
viongozi wa dini na wadau mbalimbali kutoka Wilaya ya Pangani, Lushoto, Handeni
na Tanga mjini kupitia mradi wa GBV, Mkurugenzi wa Tree of Hope , Fortunata
Manyeresa, alisema viongozi wa dini wako na nafasi kubwa ya kutokomeza ukatili
wa kijinsia maeneo yao.
Alisema vitendo vya ukatili vya kijinsia vimekuwa vikishamiri kila siku hivyo kuwataka
viongozi hao wa dini kutumia nafasi zao katika jamii kuhakikisha vitendo hivyo
vinakomeshwa.
“Jambo la kufurahisha hapa leo tupo na viongozi
wa dini tofauti pamoja na wanaharakati, tutumie nafasi zetu kwa kukemea vitendo
vya ukatili” alisema Manyeresa na kuongeza.
“Bado ukatili wa kijinsia kwa watoto na wazee
unaendelea hili ni jambo la kuhuzunisha na linatakikana kupingwa kwa nguvu zote
kwa kushirikiana na Serikali” alisema.
Afisa mradi Tree of Hope, Goodluck Malilo,
aliwataka wanaharakati kutoka Wilayani kuwa mabalozi wa kupambana na vitendo
vya ukatili watoto na wazee.
Alisema kwa kupaza sauti moja vitendo hivyo
vinaweza kutokomezwa hivyo kuwataka baada ya kupata maelekezo na mbinu
kuhakikisha wanawafikisha katika vyombo vya sheria wote wanaojihusisha na
ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Mwanaharakati kutoka Wilayani
Mkinga, Fidea Mtambo alisema vijijini kuna changamoto kubwa ya kupambana na
vitendo vya kikatili hivyo kuitaka Asasi hiyo kuendeleza mapambana yake kijiji
kwa kijiji.
Nae Ustadhi, Ustadhi Abdalla Mbena kutoka kata
ya Donge Tanga mjini, alisema kuna baadhi ya watu wanaofanyiwa ukatili wa
kijinsia wamekuwa waoga kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.
Alisema ili kuweza kutokomeza ni wajibu wa kila
mmoja kuwa balozi wa kupinga vitendo vya ukatili vya kijinsia katika eneo lake.
Washiriki katika kongamano hilo wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment