Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 22 January 2017

MBUNGE DODOMA.MJINI AKABIDHI MSAADA WA VIFAA TIBA JIMBONI KWAKE

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi vitanda vya hospital na vyandarua vyenye thamani ya Tsh 3,500,000 kwa Zahanati na vituo vya Afya 20 katika Jimbo la Dodoma Mjini.

Akiongea wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi vitanda hivyo,Mh Mavunde alisema amefanya hivyo ili kutatua changamoto ya ukosefu wa vitanda vya kutosha hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu kwa wagonjwa wengi pindi inapotakiwa kupatiwa huduma kwa kupumzishwa katika zahanati hizo,Akaendelea kueleza kwamba Vitanda hivi vitasaidia sana kuboresha huduma ya Afya haswa katika maeneo ya pembezoni mwa Manispaa ya Dodoma na hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa pindi wanapohitajika kulazwa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Ndg Kunambi amemshukuru Mbunge Mavunde kwa jitihada zake kubwa katika kuwahudumia wananchi wa Dodoma,na pia akaeleza kwamba tayari Manispaa ya Dodoma imeshaagiza magodoro kutoka MSD kwa ajili ya vitanda hivyo ili wananchi waanze kuvitumiq mara moja.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment