Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi, Alhaj, Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Apili 11, 2018.
Waombolezaji wakishiriki katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM wa mkoa wa Lindi, Alhaj Ali Mtopa kwenye
kijiji cha Nanjilinji wialyani Kilwa Aprili 11, 20918.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na waombolezaji katika mazishi
ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM Mstaafu wa Mkoa wa Lindi,
Alhaj, Ali Mtopa katika kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Apili 11,
2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki katika sala ya kumwombea
Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM mkoa wa Lindi, Alhaj
Ali Mtopa wakati aposhiriki katika mazishi ya Mwansiasa huyo
yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nanjilinji wilayani Kilwa, Aprili 11,
2018.
Waombolezaji wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe na Mwenyekiti wa CCM
Mstaafu wa mkoa wa Lindi, Alhaji Ali Mtopa kwenye kijiji cha Nanjilinji
wilayani Kilwa Aprili 11, 2018.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameiasa jamii nchini kujiepusha na migogoro kwa
vile haina tija na badala yake idumishe amani, upendo na
uadilifu ili kumuezi mwanasiasa mkongwe nchini, marehemu Alhaj Ali
Mtopa.
Aliyasema hayo jana (Jumatano, Aprili 11, 2018) alipomuwakilisha
Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika katika
kijijini Nanjilinji wilayani Kilwa. Alhaji Mtopa alifariki Jumatatu Aprili 9
jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu alisema haitapendeza kusikia jamii, wanafamilia,
watendaji au wanasiasa waliokuzwa au kufunzwa na marehemu Alhaj Mtopa
wakifarakana kwa sababu yoyote ile kwani siku zote marehemu alikuwa
kiongozi aliyejitahidi sana kuwawaunganisha watu na mpenda amani.
“Tumepoteza kiongozi maarufu mwenye historia pana, amekuwa
mtumishi ndani chama (CCM) na Serikali kwa muda mrefu. Alikuwa kiongozi mwema
muadilifu, mtiifu na mchapakazi kwa miaka mingi”.
“Marehemu Alhaj Mtopa hakua mbaguzi kwenye kuielimisha jamii namna
ya kuendesha siasaza kistaarabu. Kifo chake kinatuacha na huzuni, kazi yetu
kubwa ni kumuombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuilaza roho yake mahali pema”.
Alisistiza Mheshimiwa Majaliwa.
Pia Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi wanafamilia kuwa
watulivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na baba ambaye alikuwa nguzo
ya familia na jamii. Hivyo aliwaomba kutoruhusu mgawanyiko wa aina yoyote baina
yao.
“Katika kipindi hiki kigumu ambacho tumeondokewa na mzee wetu na
mwalimu wetu wa siasa na uongozi wetu nawasihi sana wanafamilia kuwa watulivu
kwani haitapendeza kusikia kuwa kuna mgogoro au mgawanyiko kati yenu”.
Alisema yeye binafsi amepata msaada mkubwa kutoka kwa maremu
Alhaj Mtopa katika masuala ya siasa na kijamii kwa vile mara nyingi akiwa katika ziara zake mkoani
Lindi na katika jimbo lake la Ruangwa aliambatana na marehemu na kwa pamoja
walishirikiana kutatua kero na kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo.
Mbali na Waziri Mkuu viongozi wengine waliohudhuria mazishi
hayo, ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Mbunge
wa Mtama, Napa Nnauye na Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Godfrey Zambi.
Wengine ni Mke wa Rais wa Awamu ya Nne na Mbunge wa Kuteuliwa
Mama Salma Kikwete, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia na Pamoja na Waziri
wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mbunge wa Kilwa Kusini,Selemani Ally Bungara na
Mbunge mstaafu wa Mtama, Benard Membe.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment