MTOTO Michael
Kadungala (15) mwenye ulemavu wa kutoona amemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dk. John Magufuli amsaidie aweze
kupata matibabu ya tumbo kujaa maji.
Kadungala
ambaye mpaka sasa ameshatoa zaidi ya lita 100 za maji katika tumbo lake lakini
maji bado yamejaa katika tumbo hilo.
Akizungumza
kwa taabu na Waandishi wa Habari,nyumbani kwa Mjomba wake,Joshua Msemwa eneo la
Ipagala Mkoani hapa,Kadugula alisema anapenda kusoma lakini anashindwa kutokana
na tumbo lake kujaa maji.
Alisema
alikuwa akisoma katika shule ya wasioona ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani
hapa lakini alirudishwa nyumbani kutokana na tumbo kujaa maji.
“Mheshimiwa
Rais mimi sioni na wewe ni Rais wa wanyonge nataka kurudi shuleni,naumia sana
ninapoona wenzangu wanaenda shule, naumia sana naomba nisaidie niweze kupata
matibabu,nakuomba sana,”alisema huku akilia.
Kwa upande
wake Mjomba wake,Joshua Msemwa alisema Kadugula alianza kuumwa 2014 na
walimpeleka katika Hospitali ya St Gasper ya Itigi na kutoa lita 28 za maji
tumboni.
Alisema
mwaka 2015 walimpeleka katika hospitali ya St Gemma ya Mkoani Dodoma ambapo
alipimwa na kuonekana hasumbuliwi na
ugonjwa wowote.
Msemwa
alisema mwaka 2017 ilibidi wampeleke
Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili na
kupimwa kila kitu lakini hakuna kitu chochote kilichoonekana.
“Zaidi ya
kupewa dawa za TB,lakini kila siku amekuwa
akitolewa maji tumboni namuonea huruma sana Mjomba wangu kwani haoni,Hivi karibuni tulimpeleka
katika Hospitali ya Benjamini Mkapa walipima kila kitu lakini hakuna kilichoonekana,”alisema
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya wasioona ya Buigiri Wilayani Chamwino,Happines Mgombela
alisema,Kadugula alishindwa kuendelea na masomo mwaka 2014 akiwa darasa la nne
kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kujaa maji.
“Sasa hivi
ndio angekuwa akimaliza darasa la saba kiukweli darasani alikuwa yupo vizuri
alikuwa akishika nafasi tano za juu hasa mbili au tatu,”alisema
Naye Mbunge
wa Jimbo la Kilolo,ambaye pia ni Balozi wa wasioona nchini,Venance Mwamoto alisema amejitahidi kwa kila hali kuhakikisha
Kadugula anapata matibabu lakini kwa sasaamefikia mwisho.
Kutokana na hali
hiyo,Mwamoto amemwomba Rais Rais Dk.Magufuli na wadau mbalimbali wamsaidie
ili mtoto huyo aweze kupatiwa matibabu.
Kauli hiyo
pia inaungwa Mkono na Diwani wa Kata ya Buigiri Keneth Yindi (CCM).
Yeyote Mwenye kuguswa kwaajili ya kumsaidia mtoto huyu Matibabu awasiliane na Mjomba wake 0755090234 JOSHUA MSEMWA.
Yeyote Mwenye kuguswa kwaajili ya kumsaidia mtoto huyu Matibabu awasiliane na Mjomba wake 0755090234 JOSHUA MSEMWA.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment