Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza wakati wa Warsha ya Wadau wa Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
Waziri wa Nishati dkt. Merdad Kalemani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua wakiteta jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
Naibu wa Nishati, Subira Mgalu na Mkuu wa mkoa Iringa Amina Masenza wakiteta jambo wakati wa Warsha ya Wadau wa Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani
Waziri
wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (kushoto) Naibu waziri wa Nishati (katikati) na
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (kulia) wakiwa nje ya ofisi ya mkuu wa
mkoa wa Iringa.
washiki
wa Warsha ya Wadau wa Mradi wa kuzalisha
umeme Rufiji wa Megawati 2100 iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
mkoani Iringa.
Na
Zuena Msuya , Iringa
Waziri
wa Nishati Dkt.Kalemani amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa,Vijiji na wadau
mbalimbali kuwaelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa kutunza na kulinda vyanzo
vya maji nchini ili yatumike kuzalisha umeme mwingi na pia katika matumizi bora
ya Kilimo cha umwagiliaji.
Dkt.Kalemani
alisema hayo wakati wa Warsha ya Wadau wa
Mradi wa kuzalisha umeme Rufiji wa Megawati 2100 inayofanyika katika
ukumbi wa Siasa ni Kilimo mkoani Iringa.
Warsha
hiyo ilishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Viongozi
wa Serikali za Mitaa na Vijiji ili kupata Elimu kuhusu faida na umuhimu wa kutunza
vyanzo vya maji yanayoingiza maji yake katika bonde la Mto Rufiji patakapojengwa
Mradi wa Kuzalisha Umeme wa megawati 2,100 kwa kutumia maporomoko ya maji
katika Bonde la Mto Rufiji.
Katika
warsha hiyo, Dkt.Kalemani alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa Mradi mkubwa wa
kuzalisha umeme kwa kutumia Maporomoko ya Maji katika bonde la Mto Rufiji, ni vyema
Wananchi wakaelimishwa umuhimu wa kutunza maji kwa ajili ya Nishati ya umeme
pamoja na matumizi mengine ikiwemo kilimo ili shughuli hizo zitekelezwe kwa
pamoja pasipo kutokea athari yoyete.
Aliweka
wazi kuwa mbali na Mradi huo kuzalisha umeme, pia eneo hilo litakuwa kivutio
kikubwa cha utalii kwa kuwa lipo katika hifadhi ya Taifa ya mbuga ya wanyama ya
Selou pamoja hivyo kungizia Serikali
mapato yatokanayo na utalii pamoja na biashara zitazokuwa zikiendeshwa katika
eneo hilo.
Vilevile
alisema kuwa Wizara zote zitashirikiana kutekeleza Mradi huo kwakuwa
utekelezaji wake unahusisha Wizara mbalimbali zikiwemo Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na Wizara ya Ujenzi,
uchukuzi na Mawasiliano .
Alieleza
zaidi kuwa hadi kufikia kwezi Julai
mwaka huu Mkandarasi atayetekeleza Mradi huo atakuwa amekwishapatikana na
kuanza ujenzi wa mradi huo utakaokamilika kwa kipindi cha miaka 3, ambapo
pamoja na mambo mengine kinachofanyika Sasa katika eneo la mradi huo ni ukamikishaji
wa miundombinu ya Barabara, Reli , Maji pamoja na Umeme vitakavyotumiwa na
mkandarasi wakati wa kutekeleza Mradi huo.
Nae
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, alieleza kuwa Mradi huo ni fursa kubwa ya
ajira za muda mfupi na zile za muda mrefu kwa watanzania wenye taaluma husika
na wale walio na uwezo na ujuzi.
Amewataka
watanzania hasa Vijana kuchangamkia fursa hiyo katika kujiletea maendeleo yao
na Taifa kwa ujumla.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza aliahidi kutoa elimu kwa
Wananchi wa Mkoa wa Iringa ambao sehemu kubwa ya mito yake hutiririsha maji
katika Bonde la Mto Rufiji.
Aidha
alisema kuwa ataendelea kuwaelimisha Wakazi wa Iringa kuweka njia Bora za
kilimo cha umwagiliaji zitakazotumika katika kilimo badala ya ile iliyozoeleka ya
kulima Vinyungu katika vyanzo vya maji
na Maeneo Oevu.
Kwa
upande wao Wabunge wa Mkoa huo akiwepo Mbunge wa Mafinga mjini, Cosato
Chumi na mbunge wa kilolo Venance
Mwamoto walisema kuwa watahakikisha Mradi huo unatekelezwa na hakutakuwa na
changamoto zitakazoweza kuukwamisha Mradi huo kuanzia hatua za awali Hadi
mwisho.
Walisema
kwa kutumia nafasi zao watawashirikisha Wabunge wenzao kuhamasisha na kusimamia
utekelezaji wa Mradi huo wenye manufaaa makubwa kwa Wananchi na Taifa kwa
jumla.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment