Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Wednesday 7 March 2018

BUNGE LAMLILIA DK WALID KABOUROU



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametuma salamu za Rambirambi kwa Mkuu wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga, kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Dkt. Aman Walid Kabourou kilichotokea usiku wa tarehe 6 Machi, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akitibiwa.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Dkt. Aman Warid Kabourou, natoa pole kwa familia ya marehemu, wakazi wa Mkoa wa Kigoma pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kumpoteza kiongozi huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Binafsi nimesikitika kumpoteza Dkt. Kabourou ambaye nilipata kuhudumu nae katika Bunge la Saba mwaka 2000 – 2005, alikuwa ni Mbunge mwenye weledi mkubwa na mawazo mazuri ya kulijenga Taifa,” alisema Mheshimiwa Spika.

Mheshimiwa Spika amemuomba Mwenyezi Mungu awape subira, nguvu na faraja familia, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mpendwa wao.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment