Mhandisi Mahenda S. Mahenda, Meneja wa Vituo vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro Systems, vinavyohusisha inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani
Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye
uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Korogwe
VITUO
vya uzalishaji umeme wa maji vya Pangani Hydro
Systems, ambayo inahusisha vituo vitatu, New Pangani, kilichoko wilayani
Muheza, Hale wilaya ya Korogwe, na Nyumba ya Mungu wilaya ya Mwanga, vyenye
uwezo wa kuzalisha umeme jumla ya Megawati 97, viko katika hali nzuri, Meneja
wa vituo hivyo, Mhandisi Mahenda S. Mahenda, amesema Leo Desemba 18, 2017.
Hata
hivyo amesema, mashine moja kati ya mbili kwenye kituo cha Hale, haifanyi kazi
na iko katika matengenezo. “Niwahakikishie tu kwamba matengenezo hayo ambayo
bado hayajaanza hayataathiri upatikanaji umeme kwa sababu vyanzo vya umeme
vimeongezeka.” Alisema.
Akifafanua
zaidi Mhandisi Mahenda alisema, New Pangani Falls inazalisha umeme Megawati 68,
Hale Megawati 21, na Nyumba ya Mungu Megawati 8 na uwezo wa vituo kutoa umeme
wa kutosha.
Akizungumza
na Wahariri wa vyombo vya habari waliotembelea vituo vya Hale na New Pangani
Falls Mhandisi Mahenda, alisema, kituo cha Hale kilijengwa mnamo mwaka 1961 na
kuanza kufanya kazi mwaka 1964 na kuwa kituo cha kwanza kabisa cha kuzalisha
umeme wa maji katika historia ya nchio yetu.
“
Utaona umri wa mitambo hiyo ni miaka 53, na moja ya mashine hizo imeharibika na
kufanya uwezo wa kituo wa kutoa Megawati 21, kupungua hadi Megawati 8, lakini
niwahakikishie wananc hi licha ya upungufu huo, bado TANESCO inao uwezo wa
kuzalisha umeme unaohitajika, kwani vyano vya umeme vimeongezeka.” Alisema.
Valvu ya kupitisha maji yanayopelekwa kwenye mashine za kufua umeme, kwenye kituo cha nguvu za umeme cha Hale ikivuja. Mhandsi Mahedna alielezea hali hiyo kuwa haina taathira kubwa na inatokana na mashine hizo kuwa na umri mrefu Zaidi.
Bwawa la maji Pangani Pangani Falls.
Mhandisi Mahenda akifafanua mambo mbalimbali ya kiufundi kwenye chumba cha kudhibiti mifumo ya umeme cha New Pangani Falls.
Exciter, moja kati ya mashine mbili ya kufua umeme kwenye kituo cha Hale, ambayo inafanya kazi.
Wahariri na wataalamu wa TANESCO, wakitembelea New Pangani Falls.
Mhandisi Mkuu wa Pangani Hydro Systems, Lewis Loiloi, akitoa maeelzo kuhusu masuala ya kiusalama kwa wahariri wakiwa kwenye handaki, la New Pangani Falls.
Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha New Pangani Falls cha 132 kV.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment