Na Katuma Masamba, Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kabla ya Desemba 30, mwaka huu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) itaanza kutoa matibabu ya kupandikiza figo ikiwa ni hatua ya kupunguza wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi.
Ummy ameyasema hayo wakati akichangia Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2017/2018 ambapo amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakibeza juhudi mbalimbali za serkali katika kuboresha huduma za afya.
Amesema kwa sasa Hospitali ya Taifa Munimbili kupitia taasisi zake kwa kiasi kikubwa imepunguza wagonjwa waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi.
Amesema kipndi cha nyuma Hospitali ya Muhimbili ilikuwa ina uwezo wa kuwafanyia upasuaji watoto 15 kwa wiki lakini sasa hivi ina uwezo wa kuwafanyia watoto 50.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment