Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 9 September 2017

KATIBU MKUU WA CHADEMA NAE ATAKIWA POLISI, MAGARI NANE AINA YA NISSAN YAKAMATWA




Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji
Na Mroki Mroki, Dodoma
JESHI la Polisi Mkoani Dodoma linamtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyetajwa kwa jina moja la Adam,pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji  kujitokeza na kufika Polisi Dodoma kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP Gilles Muroto amesema dereva huyo anatakiwa kufika katika ofisi yake bila kukosa au Makau Makuu  ya Polisi jijini Dar es Salaam ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio hilo.

“Jeshi la Polisi linamataka dereva wa Tundu Lissu aitwae Adam ambaye alikuwa nae siku ya tukio, afike kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo kwakuwa ndiye aliyekuwa pamoja na majeruhi wakati wa tukio,”alisema Muroto.

Polisi pia limemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Vicent Mashinji kufika kituo cha Polisi Dodoma au katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Dar es Salaam kwa mahojiano.

Aidha Polisi mkoa wa Dodoma linayashikilia magari nane aina ya Nissan pamoja na madereva wake kwa mahojiano kuhusiana na magari hayo kuhisiwa kuhusika katika tukio la shambulizi la Mbunge wa Singida, Tundu Lissu.

Aidha amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na msako mkali wa watuhumiwa waliohusika katika tukio la kumshambulia Mbunge Tundu Lissu nyumbani kwake.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment