Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Sunday 10 September 2017

SERIKALI YATAKIWA KUTUNZA BARABARA ZAKE

SERIKALI imetakiwa kuweka mkakati wa kuzilinda, kutunza na kuhifadhi   barabara zote zinazojengwa kwa kiwango cha lami nchini ili kuziwezesha kudumu kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuepuka gharama za ukarabati wa mara kwa mara.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mheshimiwa Moshi Suleman Kakoso amesema hayo mara baada ya kukagua barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilomita 263, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika.

“Hakikisheni ujenzi wa barabara unaendana na uboreshaji wa huduma na maisha ya wananchi sehemu ambapo barabara hizo zinapita ili kuchochea maendeleo”, amesema mheshimiwa Kakoso.

Makamu mwenyekiti huyo amesema Kamati yake imeridhishwa na hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara Dodoma –Babati KM na daraja la Kelema linalounganisha Wilaya za Chemba na Kondoa ambalo litawezesha barabara hiyo kupitika kwa uhakika wakati wote. 

"Nimefurahishwa na taarifa aliyoitoa Meneja mradi wa barabara hii kwamba pamoja na kujenga barabara pia mkandarasi amechimba visima vya maji katika maeneo haya kwa ajili ya kusaidia wananchi jambo ambalo ni jema na la kuigwa na makandarasi wengine”, amesisitiza Makamu Mwenyekiti Kakoso.
Aidha, Makamu Mwenyekiti ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi),  kuwa na mpango endelevu wa kuweka kingo zinazoonesha mipaka ya hifadhi ya barabara mapema na kwa uwazi ili kuepusha migogoro kwa wananchi na ulipaji wa fidia zinazoweza kuepukika.

Ameongeza kuwa Serikali ihakikishe inasimamia ipasavyo sheria zinazolinda barabara ikiwemo kuweka alama za vivuko vya wanyama mahala panapostahili ili kudhibiti mifugo kukatiza ovyo katika barabara.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema katika kuhakikisha kuwa Serikali inailinda barabara ya Dodoma - Babati tayari imeagiza uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara kuhakikisha wanatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa mizani ili kudhibiti madereva wanaozidisha uzito usiokubaliwa kisheria.
Ameongeza kuwa Wizara inaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhamasisha utunzaji wa miundombinu ya barabara kama kutomwaga mafuta barabarani,kutopitisha mifugo na kutoiba alama za barabarani.

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu imefanya ziara katika mradi wa barabara ya Dodoma - Babati (Km 263), na daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 lililopo wilaya ya Chemba mkoani.

Dodoma na kuridhishwa na miradi hiyo ambapo wameitaka Serikali kupitia wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kuhakikisha inalinda na kutunza miundombinu hiyo ili idumu muda mrefu.
Muonejano wa Daraja hilo kwa chini.


 Wajumbe wa Kamati wakipiga picha ya pamoja baada ya kukamilisha ziara yao.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment