Spika wa Bunge la Tanzania; Job Ndugai (kulia) akipokea mwaliko maalum wa kujiunga na Umoja wa hiari wa Mabunge ya Afrika (APU) kutoka kwa Mwenyekiti wa umoja huo na Spika wa Bunge la Guinea Bisau; Cipriano Cassama katika ofisi ndogo za Bunge; Dar es Salaam jana. (Picha na Mroki Mroki).
Spika Ndugai akiwa na Mgeni wake Spika wa Bunge la Guinea Bisau, Cassama.
BUNGE la Tanzania limepokea mwaliko
kutoka kwa Spika wa Bunge la Guinea Bissau, Cipriano Cassama wa kujiunga kwenye
Umoja wa hiari wa Mabunge ya Afrika (APU) ambao wanaongea lugha nne na
kuwapatia vitendea kazi, kanuni na taratibu za kujiunga.
Mbali na Cassama ujumbe huo pia
uliambatana na Katibu Mkuu wa APU, NZI Koffi na wawakilishi wengine kutoka nchi
za Ghana na Senegal.
Ndugai alisema ‘’bunge hilo linatumia
lugha za Kifaransa, Kireno, Kiarabu na Kiingereza ambapo ni tofauti na bunge la
Jumuiya ya Madola tulilojiunga nalo ambalo linatumia lugha moja pekee ya
Kiingereza.’’
Alisema kuwa taratibu wa kujiunga na
umoja huo utafanyika na kwamba watajibu mualiko huo mapema iwezekanavyo.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment