Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Thursday 24 August 2017

MAVUNDE AZINDUA PROGRAMU YA KUKUZA UJUZI KWA VIJANA MTWARA.

 NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Anthony Mavunde akisikiliza vijana
 NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Anthony Mavunde akishiriki moja ya kazi za vijana hao
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu- Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Anthony Mavunde  amezindua Mafunzo ya Utambuzi wa Ujuzi uliopatikana nje ya mfumo Rasmi,  kwa Vijana 847 kutoka Mikoa ya Mtwara, Lindi, Morogoro, Pwani, na Dar es Salaam mafunzo yaliyozinduliwa Mkoani Mtwara. 

Mavunde amewataka Vijana kuutumia ujuzi watakaoupata kupitia mafunzo hayo ili waweze kujiajiri na kuajiri Vijana wengine na pia kutumia ujuzi huo kushiriki katika Uchumi wa Viwanda.

Mavunde aliwataka Vijana waliopata fursa ya kuingia kwenye Mafunzo Haya, kutumia vizuri fursa hii kwa kuwa Waaminifu na Kuwajibika  ipasavyo ili kujenga msingi wa mafanikio.

"Mafunzo haya yanatolewa na Serikali kupitia Fedha za walipa kodi  hivyo mhakikishe fursa hii vyema ili iongeze thamani katika shughuli zenu,Serikali ya Mhe John Pombe Magufuli imedhamiria kuwekeza kwa vijana kwa kuwajengea ujuzi  vijana na kuwawezesha  ili waweze kushiriki katika Uchumi wa Nchi yao"Alisema Mavunde

Vijana washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuthamini vipaji  vyao vya ufundi kwa kuwaongezea Ujuzi na kuwarasimisha kwa kuwapatia vyeti vya Mafunzo ya Ufundi pasipo wao kupitia vyuo vya Ufundi katika utaratibu wa kawaida wa masomo.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment