Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 26 June 2017

MIKOA 14 KUANZA KUPATIWA VIUADUDU KUANZIA LEO



AGIZO la kuhakikisha Halmashauri zote nchini zinachukua dawa za viuadudu zinazozalishwa kwa katika kiwanda cha dawa hizo kilichopo Kibaha, Pwani imeanza kutekelezwa kwa Halmashauri za mikoa 14 kutakiwa kufika katika kiwanda hicho na kuchukua dawa hizo. Anaandika Frank Shija-MAELEZO

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Msemaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto –Idara Kuu ya Afya, Catherine Sungura, imesema kuwa Viuadudu hivyo vitaanza kugaiwa katika Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.

“Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu anapenda kuwatangazia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa Viuadudu vitaanza kugaiwa leo Juni 26, 2017 kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa Malaria” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Mikoa inayoanza kupata mgao huo, na iwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria kwenye mabano kuwa ni pamoja na Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%).

Taarifa hiyo imebainisha kuwa mikoa mingine ambayo haijatajwa itagaiwa Viuadudu katika awamu ijayo.

Aidha taarifa hiyo imewakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufanya upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini.

“Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Rais John Pombe Magufuli alitoa agizo hilo akiwa katika hafla ya uzinduzi wa barabara ya Bagamoyo – Makofi – Msata wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Pwani iliyoanza tarehe 21 hadi 23, mwezi Juni 2017, ambapo alitoa siku 7 kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha zimechukua dawa hizo ambazo yeye amezilipia.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment