Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Monday 26 June 2017

MAVUNDE AWAHIMIZA WAISLAMU KUMUOMBEA RAIS MAGUFULI.

 NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde (katikati) akiwa katika baraza la Eid el Fitr Mkoani Dodoma.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Anthony Mavunde amewaomba waamini wa dini ya kiislamu na watanzania kumuombea Rais Dk.John Magufuli ili Mwenyezi Mungu amjaze Ujasiri, Hekima na Maarifa.

Akizungumza leo katika Baraza La Eid el fitr Mkoa wa Dodoma lililofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma lililoongozwa na Sheikh wa Mkoa huo, Mustafa Shaban Rajab, Mavunde amesema ni vyema watanzania na waumini hao kumuombea Rais kwa kuwa anadhamira ya kweli ya kuwatumikia watanzania.

Mavunde ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, amesema maombi zaidi yanahitajika hasa katika kipindi hichi cha kupambana rushwa, ufisadi na vita dhidi ya Uhujumu uchumi.

“Waislamu na watanzania kwa ujumla wenye mapenzi mema na Taifa hili ni vyema mkamuombea Rais wetu ili aendelee kuliongoza Taifa Tanzania na kupambana na vitendo viovu vinavyorudisha nyuma Taifa kimaendeleo,”amesema Mavunde
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwatakia Waislamu wote heri ya sikukuu ya Eid na kuwaomba viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri kuhusu Upendo, Umoja na Mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali tofauti ya itikadi za vyama,dini, rangi wala kabila.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment