WANAFUNZI wawili wamekufa hukubabiria wengine 24 wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika enwo la Banda la Ngozi jijini Dar es Salaam leo. Anaandika Katuma Masamba.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema, ajali hiyo imetokea leo saa 12:30 asubuhi ambapo imehusisha lori aina ya Scania lenye namba T273 CEV na daladala aina ya Eicher lenye namba T376 DFT ambayo yaligongana uso kwa uso.
Kamishna Sirro amewataja wanafunzi waliokufa katika ajali hiyo ni Itlam Wema Athuman ambaye ni mwanafunzi wa Kidato cha kwanza shule ya Sekondary Msimbazi na Sakina Hamis Imamu mwanafunzi wa shule ya sekondari Mchikichini.
Amesema kati ya majeruhi 24 tisa ni wanawake na 15 ni wanaume na najeri 21 kati yao wamepata matibabu na kuruhusiwa.
Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba T.273 CEV scania mali ya kampuni ya Mikoani Traders kuingia barabara ya pili bila kuchukua tahadhari kwa nia ya kuingia kwenye maegesho ya ofisi yao na kusababisha ajali hiyo.
Aidha alisema dereva wa lori hilo Isack Moshi amekamatwa kwa mahojiano zaidi na magari yote mawili yapo katika kituo cha Polisi Chang’ombe huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya Temeke.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment