Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.

Have you got a good story?

Share your story, discuss the issues with Dailynews Blog.





Nafasi Ya Matangazo

Saturday 27 May 2017

VIGEZO KUZINGATIWA KWA WANAFUNZI WANAOKWENDA KUSOMA VYUO NJE YA NCHI

 Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Dk.Fabian Mahundu akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India Nchini Tanzania, Sandeep Arya  akizungumza akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozi wa India Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Udahili wa Global Education Link (GEL), Zakia Nassor akitoa elimu kwa wanafunzi waliotembelea banda  katika maonesho ya vyuo Vikuu vya nchini India vilivyofanyika katika Ubalozini  Jijini Dar es Salaam.
Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk.Fabian Mahundu akiwa na Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa  Global Education Link (GEL), Abdulmaalik Mollel wakitembelea  mabanda katika  maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India.leo jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya akiwa katika picha ya  watanzania  25 waliopata ufadhili wa Serikali ya India wa kusoma katika vyuo vikuu vya nchi hiyo leo jijini Dar es  Salaam.
TUME ya Vyuo  Vikuu Nchini  (TCU) imesema kuwa wanaokwenda  kusoma vyuo vikuu vya nje wanatakiwa  kuangaliwa vigezo ambavyo vinahitajika.

Hayo yamesemwa na Afisa Udahili Mwandamizi wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Dk. Fabian Mahundu wakati wa maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yaliyofanyika katika ubalozi wa nchi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

Dk. Mahundu amesema mwanafunzi anayekwenda kusoma vyuo vya nje na ndani anatakiwa kuwa ufaulu wa D mbili ambazo ni viwango vilivyowekwa.

Amesema kuwa mwanafunzi anayekwenda kusoma nje bila kupita katika  tume hiyo ilivyowekwa kwa ajili ya kuratibu,  akirudi anakuwa anakosa sifa katika mfumo wa elimu nchini.

Kwa upande wa Balozi wa India nchini, Sandeep  Arya amesema kuwa Tanzania na India zimekuwa na mahusiano mazuri katika nyanja mbalimbali.
Amesema India imekuwa ikitoa elimu bora na kwamba Tanzania ni nchi ambayo inanufaika kwa kupata ufadhili wa watu 25 kila mwaka.

Naye, Mkurugenzi wa Global Education Link  (GEL), Abdulmalik Mollel amesema kuwa nchi ya India  iangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya ufadhili hadi kufikia 100 kutokana na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa GEL imekuwa katika msisitizo wa mara zote katika kuhakikisha wanafunzi wote wanapita TCU  kwa ajili ya kuhakikiwa.

 Maonesho ya vyuo vikuu vya nchini India yamesimamiwa na kampuni ya Global Education Link (GEL) kwa kuteuliwa na Balozi wa India.


Kuna Maoni 0 mpaka sasa.

Post a Comment