TIMU ya Soka ya Simba ya Jijini Dar es Salaam leo imetazwa rasmi kuwa Mabingwa wa Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara (FA) baada ya kuilaza Mbao FC ya Jiji Mwanza kwa mabao 2-1 katika mtanange wa vuta ni kuvute uliochezwa kwa dika 120 katika dimba la Jamhuri Mjini Dodoma leo. Anaandika Mroki Mroki-Dodoma.
Simba na Mbao zilicheza mbele ya mshabiki lukuki kutoka mji wa Dodoma na mikoa jirani wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ambapo pia mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.
Kufuatia ushindi huo sasa
Simba itaiwakilisha nchi katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba imekuwa timu ya pili
kutwa kombe hilo la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports
Federation Cup (ASFC) tangu kuanzishwa ambapo watani zao Yanga ndio walikuwa
wakwanza kutwaa kombe hilo.
Aliyewainua viti maelfu ya
mashabiki wa Simba alikuwa ni mchezaji wa kimataifa wa Simba, mzaliwa wa Ivory
Coast, Frederick Blagnon baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza kunako
dakika ya 95 na kuamsha matumaini ya wakongwe hao wa Mtaa wa Msimbazi ya kutwaa
ubingwa wa FA.
Dakika ya 109 ya mchezo huo
mchezaji wa Mbao FC, Robert Ndaki alizima furaha za Simba uwanja wa Jamhuri na
viunga vya Mji wa Dodoma ambao tayari walianza kushangilia ubingwa kwa kuifungia
timu yake bao safi kufuatia makosa ya walinzi wa Simba na kupiga majalo iliyo
mpita mlinda mlango wa Simba.
Dakika ya 119 palitokea
piganikupige katika lango la yanga na katika harakati za kuokoa mpira mchezaji
wa Mbao aliunawa mpira na mwamuzi wa Ahmed Kikumbo kutoka Dodoma kuamuru mwaju
wa penati upige ambapo almanusra mwamuzi aambulie kichapo.
Chiza Kichuya alipiga mkwaju
wa penati kunako dakika ya 120 ishirini ambapo bao hilo lilidumu hadi kipenga
cha mwisho Simba 2 na mbao 1.
Vikosi vya timu zote mbili
vilivyoshuka dimbani hii leo ni
MBAO FC: Benedict Haule,
Asante Kwasi, Yussuf Ndikumana, David Mwasa, Salmin Hozza, Boniface Maganga,
George Sangija/Dickson Ambundo dk59/Rajesh Kotecha dk104, Jamal Mwambeleko,
Pius Buswita, Habib Hajji/Robert Ndaki dk104 na Ibrahim Njohole: KOCHA: Etienne
Ndayiragile
SIMBA SC: Daniel Agyei,
Janvier Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tahabalala’/Abdi Banda dk51, James Kotei,
Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin, Laudit Mavugo, Said
Ndemla/Frederick Blagnon dk80 na Juma Luizio/Ibrahim Hajib dk60. KOCHA: Joseph
Omong
WAAMUZI: Ahmed Kikumbo alisaidiwa na Mohamed Mkono na Omary
Juma lakini Msimamizi wa Mchezo alikuwa Florentina Zablon.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment