Kampuni ya Simu ya Tecno ikitoa msaada katika kituo cha watoto yatima
cha upendo kilichopo mkoani Mwanza. Tecno ilitoa vyakula vya thamani ya
shilindi 2.5.
*******************
Na Alexander Sanga,Mwanza
Uongozi wa kampuni ya simu za
mkononi ya Tecno imetoa msaada wa vyakula wenye gharama ya shilingi milioni 2.5
tsh kwa kituo cha kulelea watoto wasio na wazazi cha Upendo Daima kilichopo
kata ya Nyegezi katika wilaya ya Nyamagana.
Akizungumza katika kusherekea
siku ya kimataifa ya familia duniani,meneja wa kampuni hiyo kanda ya ziwa
Gerald Tito alisema kampuni yao imeamua kutoa msaada huo kwa kituo hicho
kutokana na watoto wengi wamekuwa wakihitaji misaada lakini wanakosa.
‘’Watoto wasiokuwa na wazazi
au walezi wamekuwa wanaishi katika mazingira magumu sana kutokana na kukosa
mahitaji ya muhimu kwao kama vile elimu na chakula.Tumekuja hapa kusaidia kituo
hiki kwa lengo la kusaidia jamii nzima’’ Tito alisema
Vyakula vilivyotolewa na
kampuni hiyo ni mchele kilogramu 100 kwa Unga wa Sembe, kilogramu 100 za
Ngano,Maharage na Sukari. Vitu vingine ni Sabuni za kufulia miche 500,Sabuni za
kufulia za Foma gold gramu 4000,mabegi ya shule 40 pamoja na madaftari boksi 3.
Tito aliahidi kampuni yao
itaendlea kusaidia vituo mbali mbali vya watoto yatima pamoja na watoto
wanaoishi katika mazinigira magumu.Meneja huyo alisema kampuni yao itajitaidi
kuhakikisha inasomesha baadhi ya watoto kutoka kituoni hapo.
Mkurugenzi wa kituo cha Upendo
Daima Laurent Sabini alishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao na aliomba wadau
wengine wajitokeze katika kusaidia kituo hicho.
Sabini alisema changamoto
kubwa wanayopata ni ukosefu wa ada kwa wanafunzi waliopo katika shule za
sekondari kutoka kituoni kwake na changamoto ya kuwalipa mishahara wafanyakazi
wa kituoni kwake.Sabini alisema kituo chao kwa mwezi kinatumia shilingi milioni
3.7tsh kwa mwezi kwajili ya chakula tu.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment