Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Manzese, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, ambapo leo amenza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam.
****************************
Na Ripota waMafoto Blog, Dar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mapandikizi ya upinzani na masalia ya wasaliti hawatapenya kwenye
uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama kwa kuwa njama zao
zimeshabainika.
Kimesema kina taarifa kwamba waliotimuliwa CCM nao
wanapanga safu za viongozi kwenye uchaguzi, lakini Chama
kimejipanga vizuri katika kuchuja wagombea hivyo wenye nia
hiyo hawatafanikiwa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rodrick Mpogolo, alisema
hayo jana alipozungumza na wanachama na viongozi wa Chama
katika ukumbi wa CCM kata ya Manzese wilayani Ubungo,Dar
es Salaam.
Alisema kuna mapandikizi kutoka upinzani wanajipanga
kugombea uongozi CCM jambo ambalo linafahamika hivyo
hakuna atakayepenya na hatutaruhusu 'virusi' kwa namna
yoyote ile.
Mpogolo pia aliwaonya viongozi wa CCM wanaondekeza ugomvi
ndani ya Chama na kuwataka wakatafute vyama vingine
ambavyo ni maarufu kwa kugombana hadi kutwangana ngumi.
Alisema katika mageuzi yanayofanyika sasa Chama
hakitaruhusu viongozi wa aina hiyo kuendelea kuvuruga a
mani, kuwachafua na kuwakandamiza wanachama wenzao.
Mpogolo alisema viongozi wenye hulka ya ugomvi,
kukandamiza wanachama ndio chanzo cha kupunguza kura za
CCM katika uchaguzi, hivyo Chama hakipo tayari
kuwavumilia.
''Viongozi hawa wanajulikana, kama hawawezi kubadilika,
waende wakajiunge na vyama vingine ambavyo ni maarufu kwa
kupigana. CCM tunahitaji kujenga umoja na upendo baina
yetu maana ndio silaha ya ushindi, "alisema.
Mpogolo alisema viongozi hao wameumiza wana CCM hadi
wengine wakaenda upinzani jambo ambalo kwenye CCM mpya na
Tanzania, hawana fursa ya kuendelea kutesa wenzao.
katika hatua nyingine Mpogolo aliwataka wana CCM ambao
wanamuwaza aliyekuwa Waziri Mkuu, na mgombea urais wa
Ukawa Edward Lowassa, wasipoteze muda wao kwa kuwa huu ni
wakati Rais Dk. John Magufuli.
"Naona kuna watu bado wanawaza Ukawa, wengine bado
wanafikiria mtu fulani. Ndugu zangu hii ni CCM mpya,
hakuna Lowassa wala Ukawa. Nimepita mikoa 26,Watanzania
wanasema hawataki upinzani, "alisema.
Mpogolo alipiga marufuku uendeshaji wa vikao vya
kushughulika na badala yake wafanye vikao vya kujenga
Chama, na katika kipindi hiki cha uchaguzi wa CCM,
wajielekeze kuchagua viongozi bora wasiotokana na rushwa.
Alisema CCM inatakiwa kuwa mfano katika kudhibiti rushwa
na kujenga nidhamu kwa viongozi na wanachama, ili iendelee
kuwa kimbilio la wanyonge na Watanzania kwa ujumla.
Mpogolo alisema Chama kina kazi ya kukomboa majimbo ya Dar
es Salaam yaliyokwenda upinzani, hivyo uchaguzi ndani ya
hama unapaswa kufanyika kwa umakini mkubwa ili kupata
safu za viongozi wa CCM watakaofanya kazi ya kumaliza
upinzani.
Kabla ya kuzungumza na viongozi hao Mpogolo, alikutana na
viongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kukutana na
kamati ya siasa ya Wilaya ya Kinondoni na Ubungo ambako
alipatiwa taarifa ya Chama ikiwemo maendeleo ya uchaguzi
katika ngazi za mashina.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akisalimiana na Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu UDSM, wakati alipowasili Kata ya Msasani Tawi la Mikoroshini leo jioni akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama, ambapo jana amenza rasmi katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wakifurahia maneno yaliyokuwa yakiongewa na Mpoglo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Lodrick Mpogolo, akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Msasani Tawi la Mikoroshini, wakati akiwa katika mfululizo wa ziara zake za kuimarisha Chama
Mpogolo akizungumza na wanachama.
Wanachama wa Msasani
Mpogolo akiagana na wanachama baada ya kumaliza kuhutubia.
Kuna Maoni 0 mpaka sasa.
Post a Comment